Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mahudhurio ya wananchi katika medani mbalimbali hususan katika uchaguzi kutakuwa ni kinga na mlinzi wa maslahi ya taifa la Iran na kuwa kutadhihirisha adhama ya Mfumo wa Kiislamu mbele ya macho ya maadui.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo alipokutana na maelfu ya walimu wa hapa nchini na kubainisha kwamba, uchaguzi ni miongoni mwa mambo muhimu ambayo yanatokana na fikra ya mfumo wa kidini wenye uungaji mkono wa wananchi katika Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, mahudhurio ya wananchi wote wa mirengo tofauti ya kisiasa katika uchaguzi ujao wa Rais wa tarehe 19 mwezi huu kutadhamini nguvu, adhama na kinga ya Iran na kuwa kwa mahudhurio haya, katu adui hawezi kuthubutu kuchukua hatua dhidi ya taifa hili.
Ayatullah Khamenei amebainisha kuwa, katika Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu si kwamba, Jamhuri imegandishwa na Uislamu na kama uchaguzi usingekuweko, basi hii leo kusingebakia athari yoyote ile ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kikwazo pekee cha kukabiliana na uonyeshaji uadui wa adui ni mahudhurio ya wananchi katika medani, kwani hatua hiyo inadhihirisha na kuonyesha adhama ya taifa lenye watu milioni 80 kwa nguvukazi imara, yenye akili na yenye mamilioni ya vijana na wakati huo huo kutia woga na hofu katika moyo wa adui.
Ayatullah Khamenei ameeleza kuwa, jambo la msingi na muhimu katika uchaguzi ni watu wote kujitokeza na kuelekea katika masanduku ya kupigia kura ili kuonyesha kuwa wanautetea Uislamu na mfumo unaotawala hapa nchini na hivyo kulipatia kinga taifa hili mbele ya maadui.
No comments:
Post a Comment