HABARI: Lowassa Lowassa Ahoji Uhalali wa rais kumzuia kushukuru wapiga kura

Mh. Edward Lowassa (katikati) Akizungumza na wanahabari

Mh. Wdward Lowassa leo akizungumza na waandishi wa habari amehoji uhalali wa rais kumzuia kuwashukuru wapiga kura .

Nukuu za Mh. Edward Lowassa hizi hapa
"Ni halali kwa Rais kuzunguka nchi nzima kwa kutumia gharama zitokanazo na kodi za wananchi kuwashukuru kwa kumchagua, lakini ni haramu kwa Edward Lowassa kuzunguka nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa kumchagua hata kama anatumia gharama zake za kutoka mfukoni.
Ninasema hii si sawa."

 "Ninaridhishwa sana na ukuaji wa social media (mitandao ya kijamii), kazi mnayoifanya ni njema sana.

Kikubwa ninachowaomba, msikubali kubanwa. Endeleeni na kazi ya kuuelimisha umma huu wa watanzania."

 "Ninawapongeza sana wabunge waliojitokeza kuzungumzia swala la maafa ya mafuriko yanayoendelea kutokea sehemu mbalimbali hapa nchini. Lakini pia nimehuzunishwa sana na viongozi wa serikali kutofika maeneo yaliyofikwa na madhara hayo na kuwafariji wahanga."






Video Iko Hapa mtu wangu


0 Comments:

Post a Comment