EXCLUSIVE: RAIS JACOB ZUMA KUWASILI TANZANIA LEO

Rais Zuma wa Africa Kusini akisalimiana na Rais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli walipokutana Addis Ababa , Ethiopia makao makuu ya AU.
Rais Jacob Zuma wa Africa Kusini anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi, ziara ambayo itafanyika siku mbili. 
Rais Zuma atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli. 
Pamoja na mengi yatayohusu ziara hiyo ya kikazi Wawili hao watajadili kuhusu mambo mbali mbali hususani sekta ya maji na uchukuzi. 
Hii itakuwa Mara ya kwanza kwa rais huyo maarufu barani Africa kuitembelea Taiga la Tanzania katika kipindi cha miaka kadhaa. 


0 Comments:

Post a Comment