BURUDANI: Snura anatumia mchina kujishapu!?

Hii ni shepu Snura baada kupotea kwa Kipindi kirefu. Soma anachosema hapa chini.
“Kuhusu suala la mimi kutumia Mchina, natamani sana siku moja nije na familia yangu muione. Hii ni asili yetu. Kwetu sote tumejaaliwa na mimi kama Muislamu naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa sijawahi kutumia dawa kuongeza makalio.
“Kama nimewahi, Mwenyezi Mungu anilaani na aondoe Baraka kwenye familia yangu. Sitoweza kupita nyumba hadi nyumba kuwaaminisha watu juu ya hili, ila nikinenepa kila kitu kwenye mwili wangu kinaongezeka.
“Mimi naamini kwamba, kila binadamu ameumbwa kutokana na majaaliwa ya Mwenyezi Mungu pasipokuangalia makabila. Ndio maana wapo Wachaga wenye shepu zao.” – Snura

0 Comments:

Post a Comment