Meli za Kivita za Marekani zilipokuwa zikiwasili katika rasi Korea. |
Mazoezi hayo ya pamoja yanayofanyika mara moja kila mwaka yalianza tangu Machi 1 ikiwa ni sehemu ya juhudi za washirika hao kuboresha utayari wao kwa ajili ya hali ya dharura kwenye Rasi ya Korea.
Takribani wanajeshi 290,000 kutoka jeshi la Korea Kusini na 9,700 kutoka majeshi ya Marekani walishiriki kwenye mazoezi hayo. Kikosi cha jeshi la maji kinavyoongozwa na manowari ya USS Carl Vinson nacho kilijiunga kwenye mazoezi hayo.
Mafunzo hayo yalijumuisha ushushaji wa vifaru na mahitaji kutoka kwenye vyombo vya usafiri kutoka nchi za nje na kuhusisha vikosi vyote vitatu vyenye silaha kwa mara ya kwanza.
Mazoezi ya kudhibiti eneo la kurushia makombora kwa kutumia vifaru na vikosi vya makomandoo baada ya kulipiga eneo hilo kwa mabomu na mizinga pia yalifanywa.
Marekani na Korea Kusini zote kwa pamoja zimesema zitaendelea na shughuli za doria na ufuatiliaji kwani Korea Kaskazini inaweza kuendelea na matukio ya kichokozi.
No comments:
Post a Comment