NEC yasalimu amri kwa chadema yaanza kuboresha daftari la wapiga kura




TUME ya Taifa ya Uchaguzi imesema kuwa imeanza mchakato wa kuboresha daftari la wapiga kura ili liweze kutumiaka kwenye upigaji kura ya maoni ya katiba mpya.

Aidha,  zoezi hilo linatarajiwa kutumia zaidi ya sh 279 bilioni mpaka kukamilika ingawa haijajulikana zoezi hilo litatumia muda gani kukamilika.

Hayo yalisemwa leo jijini hapa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, (NEC), Jaji Damian Lubuva alipokuwa akiongea na viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Sombetini pamoja na waandishi wa habari.

0 Comments:

Post a Comment