ASKARI Polisi mwenye namba za usajili F.5264 PC Sabato, (37), aliyeuawa Februari %, mwaka huu kwa kupigwa jiwe kichwani na mshtakiwa wa kesi ya
uvunjaji wa nyumba, Njoke Ole Kiripi (34), mkazi wa Olebomba, Wilayani longido, amesafirishwa leo , kwenda kijijini kwao Visiwa vya ukerewe Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amesema kuwa tayari taratibu zote zimekamilika za kusafirisha mwili huo.
"Leo tunaondoka ila sio mimi, tumemteua kijana mmoja wa huko Ukerewe, ili aongoze msafara kwenda kumpumzisha huyu mwenzetu na wakifika huko
taratibu zingine zitafuatwa,"alisema.
Hata hivyo Kamanda Sabas alisema kuwa wakishafikisha mwili huo kwao, taratibu zingine zitafanywa na
ndugu zake ikiwemo kupanga siku ya mazishi.
NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA ASHIRIKI MAZISHI YA NDUGU NASSOR HAMDANI TABORA
-
Na Mwandishi Wetu, Tabora
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara,John Mongella, kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migir...
5 hours ago
0 Comments:
Post a Comment