SERIKALI
imetakiwa kuchukua hatua madhubuti za kushughulikia tatizo la watendaji wabovu
ndani ya Halmashauri hapa nchini vinginevyo hata bajeti ya maendeleo ikiongezwa
na kupelekwa kwa wakati haiwezi kuleta tija kwa wananchi.
Hayo
yalisemwa jana na mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, (CCM) wakati alipokuwa
akizungumza kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa inayoendelea na vikao vyake jijini hapa.
Alisema kuwa sababu zinazotolewa na wataalam toka hazina
kuwa fedha zinazochelewa kupelekwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo
kwenye halmashauri hapa nchini ni zile zinazotolewa na wahisani na washirika wa
maendeleo hazina ukweli.
Lugola alisema kuwa kuna uthibitisho hata fedha
zinazotolewa na Serikal ambazo hukusanywa Mamalaka ya mapato nchini, (TRA) nazo
huchelewa vilevile hivyo akawataka watendaji wa hazina kubadilika kiutendaji.
“Hata mkipeleka fedha zinazotosheleza kwenye hizi
halmashauri kama mapendekezo ya bajeti zao yanavyoonyesha, tusitegemee
mabadiliko chanya kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi kama tutaendelea kuwa
na watumishi wa umma hawa hawa wanaotafuna fedha za umma kama mchwa” alisema
Lugola.
Aidha Lugola
aliitaka ofisi ya Hazina itoe maelezo ya kina juu ya utaratibu walioanzisha wa kupeleka
mabilioni ya fedha kwenye halmashauri kabla hazijapitishwa na Bunge.
“Mniambie hapa mnapata wapi madaraka haya ya
kupeleka fedha halmashauri bila sisi wabunge kuzipitisha Bungeni kama utararibu
wa kisheria unavyotaka?,”alihoji Lugola huku akitolea mfano kiasi cha shilingi shilingi
milioni 500 zilizopelekwa kwenye halmashauri ya wilaya ya Korogwe bila
kupitishwa na bunge.
Alisema
kuwa baada ya kufuatiliwa fedha hizo zilikutwa zimetumika zote kulipia posho za
madiwani na kuendesha uchaguzi jambo alilodai kuwa linadhihirisha kuwa huo ni
mwendelezo wa mtandao wa kutafuna fedha za umma.
Kwa
upande wake akifanya majumuisho Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Rajabu Mbarouk na kusema Hazina inawapasa watoe ufafanuzi, japo
wamesahampa taarifa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Alisema
kuwa ni vema halmashauri zikapanuliwa uwigo wa kukusanya mapato kwa kukusanya
kodi kwenye mabango ya barabarani, matangazo yanayodandikwa kwenye maeneo
mbalimbali pamoja na yale yanayochorwa kwenye nyumba sanjari nay ale yatayotangazwa
na magari.
Kwa upande wake,Afisa Usimamizi wa Fedha
Mkuu Hazina Arusha, Charles Mwamwaja, aliomba apewa muda wa kuzifanyia kazi
hoja hizo jambo litakalomwezesha kutoa majibu stahili.
Akijibu hoja za Wabunge hao, Naibu Waziri wa TAMISEMI,
Kasim Majaliwa alisema kuwa kwa sasa Serikali imejizatiti kushughulikia
watendaji wabovu kwenye wizara, mikoa na halmashauri nchini.
Alisema kuwa hata wale waliohusika na kashfa ya
kuchakachua fedha za umma kwa kupelekea sh milioni 800 halmashauri ya Mbozi badala
ya sh milioni 80 waliyokuwa wameomba ambao nao walizitumia ndani ya miezi
miwili tayari wameshachukuliwa hatua ambapo wengine wamesimamishushwa vyeo ili
kupisha uchunguzi zaidi wa suala hilo.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa majina yapo ila kwa wakati
huo hakuweza kuyataja kwani hayakuwa yote ambapo alisema kuwa idara nzima ya
uhasibu kwenye ofisi za TAMISEMI imewajibishwa na aliyekuwa mkurugenzi wa
halmashauri alishushwa cheo na kuwa mkuu wa idara pamoja na afisa Elimu naye
amewajibishwa.
0 Comments:
Post a Comment