Wasomaji wangu
wapenzi kwanza niwaombe radhi kwa kutowapa taarifa mpya kwa takribani zaidi ya
mwaka mmoja
Ninaowamba mnisamehe
kwani pengine sababu zilizopelekea hayo zinaweza zisipokewe kwa uzito sawa
miongoni mwenu.
Kama
mnavyoona niliweka taarifa ya mwisho October 13, kwa bahati mbaya alifajiri ya October 14, 2012 siku ya jumapili majira ya saa 11:40 dada
yangu mpenzi rafiki yangu wa karibu swahiba wangu na msiri wangu mkuu Vicky
Bahati aliondoka katika ulimwengu huu na kurudi kwa baba yetu wa mbinguni.
Kuondoka kwa
rafiki yangu huyu ilikuwa ni jambo gumu ambalo kwanza lilinishtusha sikutegemea
kama anaweza kuondoka ghafla hivyo niliumia sana kwani nilitamani ningekuwa
karibu yake nimsaidie.
Niliumia kwa
mambo mengi wakati mwingine nikijilaumu kwa nini sikufanya jitihada nifike
Iringa pengine ningeweza kumzuia Yule nesi
wa hospitali ya mkoa wa Iringa ambaye alimchoma sindano ya usingizi asifanye
hivyo.
Nesi huyo
ambaye nilipigiwa simu na mdogo wangu Charles na shemeji yangu Philemon
wakiniambia wanamuuliza anamchomaje sindano Vicky kwa maelekezo ya simu
anayopewa na dr lakini hakutaka kujibu zaidi ya kuendelea na zoezi lake la
kuchoma sindano.
Inaniuma
kwani nilitamani ningekuwepo kwani ningeweza hata kuisoma dawa anayomchoma
lakini sikuwa na uwezo wa kusafiri kwa wakati huo kwani nilikuwa mjamzito na
safari ya Arusha mpaka Iringa dr alinishauri si sahihi kiafya.
Iliniuma na
inaendelea kuniuma kwani baada ya kuchomwa sindano hiyo waliniambia Vicky ambaye
alikuwa akisumbuliwa na malaria na ilikuwa inamfanya anapoteza kumbukumbu
anaongea mambo yasiyoeleweka alilala usingizi.
Lakini baada
ya nusu saa nikapigiwa simu tena nikiambiwa niendelee kumuombea kwani anakoroma
sana nikawaambia wamweke shingo vizuri nikawaambia wajaribu kumwangalia dr wa
zamu ili aweze kumhudumia zaidi lakini jibu likawa hakuna dr ni nesi ni yuleyule
ambaye hataki kutoa majibu ya maswali anayoulizwa kuhusu afya ya mgonjwa.
Kwa keli
sikulala nilikuwa nikiendelea kuongea na Mungu wa mbinguni amponye dada yetu
huyo kwani sisi tuko watatu tu kwa mama yetu mpenzi Cecy ukimchukua tutaumia
sana, nilikuwa najua Vicky ni mpiganaji jasiri si legelege hajawahi kulazwa
hospital toka amezaliwa kwa hiyo nikazidi kumlilia Mungu kwa kuwa hii ni mara
ya kwanza kuumwa hoi amponye ili apate kuyasimulia matendo yake makuu.
Lakini Mungu
alikuwa na mipango dhidi ya Vicky Saa 11.39 asubuhi Charles ananipigia simu
akilia ananiambia Vicky ameondoka sikuamini nililia sana lakini akili yangu
ikafanya kazi mara moja mama yangu ni mgonjwa wa sukari nahitaji kuwa jasiri
ili nimnusuru na madhara ambayo yanaweza kupelekea na yeye kupoteza uhai.
Nilikuwa
nyumbani na wafanyakazi na mtoto wangu wa 4 yrs Albert Mume wangu alikuwa amesafiri nilimsikia
Vicky ananiambia “umeshakuwa sasa simama
uhakikishe kila kitu kinakuwa sawa ukweli ni huo na hakuna wa kuubadilisha” na
kweli kwa uwezo wa Mungu niliweza.
Ila mpaka
sasa bado naamini rafiki yangu yuko salama kwa baba, na naamini kila jambo ni
mpango wa Mungu hayo yaliyotokea Mungu ameyakubali kama asingeyakubali
yasingetokea.
“Ila rafiki
yangu Vicky hakuna aliyeweza kuvaa viatu vyako kila mmoja anahisi kupungukiwa wewe
ni mama bora kwa Brightness na Bakili hakuna atayeweza kuchukua nafasi yako”.
Wakati
tunaipamba nyumba yake ya milele nilijiuliza hivi haya yanaweza kubadilisha
ukweli kuwa ameondoka nikajijibu ukweli huo haubadiliki lakini kwa tabia yake alipenda
kutengeneza vitu vyake vya muonekano tofauti basi na nyumba yake aliyopumzika
tukaifanya ya kivyekovyake kama ulivyozoea kuniambia.
“Vicky sina
mtu ambaye naweza kuongea naye na simu kila saa, kuchat naye kwa msg kama vile
wala wa kuweleza huzuni, raha karaha navyokumbana navyo, japo nimejaribu
kumweleza dr kuwa bado mimic na wewe huwa tunaongea amenikatalia ananiambia ni
mawazo yangu ila mimi naamini ni wewe dada japo nilikuwa nikikuita dada
unashtuka kuwa nataka kukuomba nini leo pia nakuita dada nikiamini utacheka
kama kawaida yako”
Kwa kifupi
hiyo ndiyo ilifanya mkakosa mambo mapya kutoka kwangu naomba wale ambao hawaoni
umuhimu wa niliyoyaeleza samahani na wale ambao hawakupenda mniwie radhi na
wale walioguswa poleni ila tukimtumainia Mungu yote yawezekana.
SAFARI YA MWISHO YA MPIGANAJI VICKY MACHA LEO NYUMBANI KWAO MOSHI
Mwili wa marehemu Vicky Macha ukisaliwa ndani ya eneo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya KCMC.
Msafara kuelekea Rau mjini Moshi nyumbani kwa mume wa marehemu.
Mama wa marehemu akiaga...
Grace Macha, mdogo wa marehemu akiaga mwili.
Mtoto wa kwanza wa marehemu
Mtoto wa pili wa marehemu (picha na Mjengwa Blog)



0 Comments:
Post a Comment