Showing posts with label Polisi. Show all posts
Showing posts with label Polisi. Show all posts

 

Baada ya Ubalozi wa Marekani Kutoa Angalizo kwa Raia Wake

Jeshi la Polisi Tanzania limetolea ufafanuzi taarifa kuhusu tahadhari ya usalama iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani, ikieleza kuwa hakuna tishio kubwa la usalama katika maeneo ya visiwani na pwani kusini mwa Kisiju. 


Taarifa hiyo imekuja muda mfupi baada ya Ubalozi wa Marekani kutoa angalizo kwa raia wake kuepuka kutembelea maeneo hayo bila idhini maalum.



Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime alizungumza na vyombo vya habari, akisema, "Tunawataka wananchi kuendelea kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu. Nchi yetu iko salama na tunahakikisha usalama wa wananchi na wageni. Hata hivyo, tunafuatilia kwa karibu taarifa zinazoenea kuhusu uwepo wa tishio la kiusalama katika maeneo ya ukanda wa Pwani, hususan maeneo ya Kusini mwa Kisiju."

Awali, tarehe 21 Machi 2025, Ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari kwa raia wake kuhusu hatari inayoweza kutokea katika maeneo ya visiwani na pwani ya Kusini mwa Kisiju, Tanzania. 


Taarifa ya ubalozi ilisema, "Raia wa Marekani wanapaswa kuepuka kutembelea maeneo ya visiwa na pwani, hususan kusini mwa Kisiju, bila idhini maalum."

Kwa sasa, Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa hali ya usalama inafuatiliwa kwa karibu, na hakuna tishio kubwa linaloashiria hatari kwa raia. 


Taarifa ya Marekani iliwataka raia wake kuwa waangalifu, kuendelea kufuatilia vyombo vya habari vya ndani kwa taarifa zaidi, na kuwa na tahadhari katika maeneo yanayohusisha utalii.

Hatua za Kuchukua:

  • Epuka eneo hilo.
  • Fuata vyombo vya habari kwa taarifa zaidi.
  • Wasiliana na familia na marafiki kuhusu usalama wako.
  • Kuwa makini na mazingira yako.
  • Rejea mipango yako ya usalama wa kibinafsi.
  • Kuwa macho katika maeneo yanayotembelewa na watalii.

 



Polisi: "Hatutasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria"

Dar es Salaam, Machi 9, 2025 – Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limemkamata na baadaye kumjeruhi kwa risasi mtuhumiwa wa utekaji mtoto, Stanley Dismas Ulaya (18), mkazi wa Kata ya Nguruka, Wilaya ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumteka mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8, mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Mbezi, Ubungo, jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lilitokea Machi 6, 2025, wakati mtoto huyo aliposhuka kwenye daladala kuelekea shuleni, ndipo mtuhumiwa alimkamata na kumpeleka hadi Bagamoyo, mkoani Pwani, ambako alimficha vichakani huku akitumia namba ya simu ya mzazi iliyokuwa kwenye madaftari ya shule ya mtoto huyo kudai pesa kwa vitisho.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, alisema kuwa Jeshi la Polisi lilifanya juhudi kubwa za ufuatiliaji hadi kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa mnamo Machi 8, 2025, majira ya saa 1:00 usiku.

"Baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, mtuhumiwa alijaribu kutoroka kwa kukimbia. Askari walilazimika kupiga risasi hewani kwa tahadhari, lakini alipokaidi, walimlenga kwa risasi mguuni na pajani ili kumzuia," alisema Kamanda huyo.

Mtuhumiwa alipelekwa hospitalini kwa matibabu kutokana na majeraha aliyopata, huku hali ya mtoto ikiendelea kuwa nzuri chini ya uchunguzi wa madaktari.

Jeshi la Polisi limeendelea kulaani vikali vitendo vya utekaji nyara na limeahidi kuchukua hatua kali kwa wahusika wote kwa mujibu wa sheria. "Hatutasita kuwashughulikia wahusika wa vitendo hivi kwa mujibu wa sheria. Tunatoa onyo kali kwa wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu," aliongeza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.




Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa ya kumpata mtoto Shamimu Nasibu Ndihagule (2) ambaye alielezwa kuwa ameibiwa kutoka kwa wazazi wake, katika tukio lililotokea Januari 15, 2025 asubuhi katika kitongoji cha Kisiwani, kijiji cha Tundu, kata ya Kidodi, wilaya ya kipolisi Ruhembe.


 Mtoto huyo alichukuliwa na mtu asiyefahamika wakati akicheza na mtoto mwenzake, Josephat Natalis Jangama (3), mkazi wa kitongoji hicho.


Mtoto Shamimu alipatikana akiwa salama katika eneo la kitongoji cha Mhovu, kijiji cha Kisinga, kata ya Ruaha, wilaya ya kipolisi Ruhembe, Januari 19, 2025 asubuhi, kwenye mashamba ya miwa, baada ya kufuatiliwa na jeshi la polisi ambao walikuwa wakitekeleza msako mkali. 


Mtoto huyo kwa sasa anapatiwa matibabu na vipimo katika Kituo cha Afya Kidodi ili kuhakikisha afya yake inakuwa salama.


Jeshi la polisi limekamata mtuhumiwa mmoja, ambaye ni mganga wa tiba za asili, kama sehemu ya uchunguzi wa tukio hili. Jina la mtuhumiwa linahifadhiwa kwa sasa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amewashukuru wananchi wote waliojitolea kwa ushirikiano wao katika kumtafuta mtoto Shamimu. 


Aidha, amewataka wazazi kuongeza ulinzi kwa watoto wao ili kuepuka matukio kama haya ambayo yanaweza kuleta taharuki katika jamii.

  

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linafanya uchunguzi na kuwatafuta watu wote waliohusika katika tukio la wizi ndani ya gari aina ya Toyota Alphard lenye namba za usajili T. 340 EJR, kama inavyoonekana katika picha zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii.



Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Januari 14, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 12, 2025, maeneo ya Kaloleni Jijini Arusha. Katika tukio hilo, mtu aitwaye Goodluck Matingisa (41) anadai kuibiwa mali zake.

Kamanda Masejo alisema kuwa uchunguzi bado unaendelea na taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitafikia umma punde. "Bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hili, na taarifa zaidi zitatolewa," alisema Kamanda Masejo.

Aidha, Kamanda Masejo alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kubeba vitu vya thamani ndani ya magari yao bila kuwa na ulinzi na kuyaacha maeneo ya maegesho bila ya uangalizi wowote. "Ni muhimu kuwa na tahadhari na mali zenu, hasa mtakapoweka magari kwenye maeneo ya maegesho," alisisitiza.


Sambamba na hilo, Kamanda Masejo aliwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa kuhusu wahalifu na uhalifu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na uhalifu. 


"Tunaomba ushirikiano wa wananchi ili kuweza kudhibiti uhalifu na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake," alisema.



Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa baada ya kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa magari ya shule (School Bus) kwa kipindi cha likizo, ambacho kilitangazwa ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi wanaotumia vyombo hivyo, kimeanza kuwakamata wale wote walio kaidi agizo hilo huku kikosi hicho kikiwaomba wananchi kuweka uangalizi wa kundi hilo.



Akiongea katika zoezi hilo, Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema kuwa kikosi hicho kilitangaza zoezi hilo na kueleza kuwa wameanza operesheni za ukamataji wa magari ambayo hayajakaguliwa na kikosi hicho.



"Kwa sasa tunaanza operesheni ya kuwakamata madereva na wamiliki wa magari ambayo hayajapitia ukaguzi huu, licha ya kuwa tulishatoa taarifa mapema," alisema SSP Zauda Mohamed.



Ameongeza kuwa takwimu zinaonyesha kuna zaidi ya magari 563 ambayo yanatoa huduma kwa wanafunzi, na baada ya ukaguzi huo, imeonekana kuwa bado kuna magari 178 ambayo hayajakaguliwa.



 "Kuanzia leo Januari 13, 2025, tunaanza ukamataji wa madereva waliokaidi agizo hili," alisisitiza SSP Zauda.

SSP Zauda pia akatumia fursa hiyo kuwataka wamiliki na madereva wa magari ya shule, kupeleka magari yao katika kikosi cha Usalama Barabarani kwa ukaguzi ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi. 



"Watu wote waliokaidi watachukuliwa hatua za kisheria, kwa sababu tunataka kuhakikisha mazingira salama kwa watumiaji hawa," alisisitiza.

Sambamba na hilo, alisema kikosi hicho kinatambua kuwepo kwa kundi jipya la watumiaji wa barabara ambao ni wanafunzi wa shule za awali walioanza shule mwaka huu. Alisema, "Tunawaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwaelekeza watoto hawa kuhusu matumizi sahihi ya barabara na kuhakikisha wana wasimamizi wakati wa kwenda na kurudi majumbani."

Pia, SSP Zauda alitoa wito kwa madereva kutambua kuwa kuna kundi jipya la watumiaji wa barabara, akiwataka kuchukua tahadhari na kufuata sheria za usalama barabarani ili kundi hilo liendelee kuwa salama kipindi chote. "Ni jukumu letu sote kuhakikisha watoto hawa wanatumia barabara kwa usalama," aliongeza.




Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amesema Jeshi la Polisi limeweka mikakati madhubuti ya kudhibiti ajali za barabarani ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyokuwa akiyatoa mara kwa mara ya kuhakikisha ajali za barabarani zinadhibitiwa ipasavyo.



IGP Wambura ameyasema hayo wakati akipokea vifaa 3050 kati ya 10000 vya kupima ulevi kwa madereva kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) vilivyokabidhiwa na Mkurugenzi wa LATRA, CPA Habibu Saluo, Makao Makuu ya Polisi Jijini Dodoma Januari 6, 2025.


IGP Wambura alisema kupitia Kikosi cha Usalama barabarani watakuwa wakali kwa madereva wazembe ambao wamekuwa wakisababisha ajali za barabarani ambapo pia wataendelea kutoa elimu ili kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa salama.


"Tumeweza kuzuia uhalifu wa aina mbalimbali na sasa nguvu pia tunazielekeza kwenye usalama barabarani kwa kuwa takwimu za ajali bado zipo juu hivyo ni lazima tuwe wakali sana ili kuona sheria za usalama barabarani zinafuatwa ili kuokoa maisha ya watanzania," alisema IGP Wambura.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo amesema, utendaji kazi wao unahitaji sana ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye dhamana ya kusimamia Sheria za Usalama Barabarani na hivyo vipima ulevi hivyo vitasaidia Kikosi cha Usalama Barabarani katika kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva walevi na wazembe pindi wanapokuwa barabarani na kuendesha pasipo kuzingatia sheria.


CPA Suluo alisema uwepo wa vifaa hivyo utasaidia kupima madereva mara kwa mara wawapo barabarani jambo ambalo litasaidia kufanya barabara zetu kuwa salama.


Aidha alisema wataendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo matumizi ya mifumo katika kufanya ukaguzi wa magari ambapo kwa sasa wanaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali.


Hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo ilihudhuriwa na Makamishna wa Polisi, Manaibu Kamishna wa Polisi, baadhi ya Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi na Maofisa kutoka LATRA.

 

Dodoma – Jeshi la Polisi Tanzania limetoa taarifa kwa umma kuhusu hatua za uchunguzi wa matukio mawili makubwa yaliyojiri hivi karibuni, likiwemo tukio la kushambuliwa kwa Deogratius Tarimo Novemba 11, 2024, katika eneo la Kiluvya, jijini Dar es Salaam, pamoja na tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa huko Kariakoo Novemba 16, 2024.




Msemaji wa Jeshi la Polisi, David  Misime (DCP), amesema kuwa uchunguzi wa matukio hayo unaendelea vizuri na hatua za mwisho zinakaribia kukamilika.


“Upelelezi wa kesi hizi mbili upo katika hatua nzuri, na hivi karibuni taarifa kamili itatolewa kwa umma,” amesema DCP Misime.

Jeshi hilo limewahakikishia wananchi kuwa litatoa taarifa sahihi mara uchunguzi wa kina utakapokamilika.




.

Afariki kwa Kunywa Pombe ya Kienyeji Aina ya Gongo 


MTU mmoja, Manota Jidailifa, amefariki dunia baada ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya gongo kupita kiasi. 



Kamanda wa Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth  Magomi, amethibitisha kuwa mwili wa marehemu umeshachukuliwa na kupelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi kabla ya kukabidhiwa kwa familia kwa ajili ya mazishi.

Tukio hili limeweka wazi athari za kutisha za matumizi mabaya ya pombe, hasa pombe za kienyeji kama gongo. Jeshi la polisi, kando na kushughulikia tukio lenyewe, limejitolea kuelimisha jamii kuhusu madhara ya pombe kali na umuhimu wa kudhibiti matumizi yake.


Pia, kuna jitihada za kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa malezi bora kwa vijana. Kamanda Magomi amesisitiza ushirikiano kati ya viongozi wa dini, wazazi, na jamii nzima katika kuhakikisha kuwa malezi bora yanazingatiwa ili kuepusha vijana na mienendo hatari, kama vile matumizi mabaya ya pombe za kienyeji, na kujenga jamii yenye afya na ustawi.

During the inauguration of the Mount "A" Police Station in the Dodoma Region, Tanzania's Vice President, Dr. Philip Mpango, urged the police force to adhere to regulations and uphold the law while executing their duties.



He emphasized the importance of ethics, discipline, and accountability in maintaining law and order. 

Additionally, he commended the police force and other security agencies for their efforts in enhancing peace and security in the country.
Furthermore, the Vice President stressed the need for the police to adapt quickly to new crime-fighting techniques by embracing the use of technology, particularly in intelligence, cybersecurity, and incorporating robotics. 
He also highlighted the importance of improving licensing systems, vehicle inspections, and utilizing technology such as road cameras and body-cam jackets to curb corruption and enhance professionalism in law enforcement, thereby reducing road accidents.

Moreover, the Vice President emphasized the importance of fostering good relations between the police force and the public to effectively combat all forms of crime. 
He also called on citizens to respect the law enforcement process. He underscored the need to continue community policing initiatives.
The Vice President urged the Ministry of Home Affairs to implement recommendations aimed at enhancing criminal justice institutions, including strengthening complaint desks and providing competent personnel for investigations to improve the performance of the police force.
In response, the Minister of Home Affairs, Engineer Hamad Masauni, noted the police force's efforts in embracing various technology systems to enhance efficiency and transparency in law enforcement, in line with the President's directives.
IGP Camillus Wambura reiterated the police force's commitment to serving the government and citizens with high integrity, fairness, and ensuring that services provided are appropriate and necessary. He emphasized that the construction of modern police stations would facilitate the realization of the true purpose of the police force, as these buildings are conducive to effective duty execution.


 

Mkuu wa Polisi Jamii wilaya ya Monduli Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Rashid Nchimbi, akiongea na baadhi ya viongozi wa vijiwe vya boda boda vilivyopo wilayani humo juu ya kuwepo kwa mahusiano bora kati yao na Jeshi la Polisi, kikao hicho kilifanyika Desemba 01,2023 katika kituo cha Polisi Monduli.


Mkuu wa Polisi Jamii wilaya ya Monduli Mrakibu wa Polisi (ASP) Rashid Nchimbi amesema kwamba msingi wowote wa maendeleo unatokana na hali thabiti ya usalama.


Hayo aliyasema mapema leo Desemba 02,2023 ofisini kwake wakati anaongea na baadhi ya viongozi wa  vijiwe vya boda boda vilivyopo wilaya ya Monduli mjini.


ASP. Nchimbi alisema kwamba, sehemu yoyote ambayo haina utulivu katika usalama basi hakuna kinachoweza kufanyika hususani upande wa maendeleo.


" Kama kutakuwa na uhalifu uliokithiri itawakatisha tamaa wafanyabishara kufanya shughuli zao, hali ambayo itaathiri kipato chenu nyinyi (Madereva wa boda boda) maana hamtapata wateja wa kutoka kwenye Bar na kumbi nyingine za starehe hasa nyakati za usiku kwa kuwa maeneo hayo yatakuwa yamefungwa mapema kwa kuogopa uhalifu. 


Vile vile watu ambao ni wateja wataogopa kutembea usiku kwa kuwa watakuwa na hofu juu ya usalama wao." Alisema ASP. Nchimbi ambaye ni mkuu wa Polisi Jamii wilaya ya Monduli.


Sambamba na hilo ASP. Nchimbi alidokeza suala la usajili wa vijiwe vyao ili wahusika waweze kutambulika badala ya Kila mmoja kukaa kijiweni kiholela Hali ambayo itawasidia kuthibitiana pindi mwenzao atafanya ndivyo sivyo. 


Alisema madereva wa Boda boda ni watu muhimu katika kuimarisha usalama wilayani humo kwa kuwa huwa wanakesha mpaka asubuhi hivyo ni rahisi kwao kushuhudia matukio mbalimbali yakiwemo ya kiuhalifu na kuwezesha kutoa taarifa haraka kwa Jeshi la Polisi.


Kwa upande wake mmoja wa viongozi hao wa vijiwe vya Boda boda aliyefahamika kwa jina la Teeneger Mwinyi alisema kwamba,  wanatamani kuwe na mkutano baina ya Jeshi hilo na wao ili na madereva wengine wapate elimu hiyo na hatimaye kuwa kufanya kazi kwa pamoja kwa nia ya kutokomeza uhalifu.


Wilaya ya Monduli mjini ina jumla ya vijiwe 14 vya madereva wa Boda boda ambavyo vimegawanyika katika maeneo mbalimbali.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Salim Hamduni



 


 








Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili Arusha na kuwabadilikia baadhi ya polisi na kuwataka kufanya kazi kwa kutenda haki pasipo kujali rangi ya mtu pia amewaonya polisi waonaokwenda kinyume na utaratibu.
Sirro amewataka polisi wanaokwenda kinyume na utaratibu wa jeshi hilo kuacha mara moja na kuwakumbusha kutenda kazi pasipokumuonea mtu ili kutenda haki kwa wananchi wote na kuleta usawa na kudai yoyote atakayebainika kwenda kinyume na utaratibu hatua zitachukuliwa ikiwemo kushtakiwa kijeshi.
Mbali na hilo IGP Sirro amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuweza kupata taarifa zinazohusiana na uhalifu na wahalifu kwa wepesi zaidi.