Wednesday, August 20, 2025

Dkt Makalla: Uelewa wa tiba mbadala umeongezeka




Na Mwandishi wetu, Doha

Mkurugenzi Mtendaji na Daktari wa kampuni ya Norland Global Tanzania, Dkt Moses Makalla amesema uelewa wa watu wengi juu ya umuhimu wa tiba asili/mbadala umechangia ufanisi wa ukuaji wa sekta ya afya Tanzania.



Akizungumza na waandishi wa habari nchini Qatar ambako yupo kwa ajili ya kutoa mafunzo na kutibu wananchi wenye changamoto mbalimbali za kiafya, Dkt Makalla ambaye kampuni yake inajihusisha na utafiti, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za tiba mbadala amesema mafanikio makubwa yamepatikana kutoka kwa watumiaji wa sehemu mbalimbali kwa kutibu chanzo cha tatizo ikiwemo magonjwa yasiyoambukiza.



“Bidhaa zetu zinatengenezwa nchini China ambako ni makao makuu ya kampuni hii, bidhaa hizi zimekuwa na msaada mkubwa na kutegemewa kuanzia nchini China mpaka katika bara la Afrika hususani kwa nchi za Afrika Mashariki kwa wagonjwa na watumiaji wake “, alisema Dkt Makalla.


Kwa mujibu wa Dkt Makalla aliweka wazi kuwa licha ya Norland Global Tanzania yenye ofisi zake katika jiji la Arusha, Dar es Salaam na Doha nchini Qatar, pia wana mipango ya kufungua ofisi nyingine katika majiji ya Dodoma, Mwanza na Mbeya kwa kuanzia.


Dkt Makalla alisema wamekuwa wakipokea wagonjwa na watumiaji wa bidhaa hizo kutoka katika mikoa mbalimbali, hivyo wameona kuna kila sababu ya kuwasogezea huduma katika mikoa ya karibu nao.


“Ninafarijika kusema kuwa Watanzania wameanza kuelewa shughuli zetu kwani tunatoa vipimo kabla ya kuhudumia mgonjwa ili tuweze kubaini tatizo alilo nalo na kumpatia tiba sahihi”, alisema na kuongeza kuwa afya ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu. 


Mbali na kufurahishwa na mrejesho kutoka kwa wagonjwa na watumiaji wa tiba na dawa hizo za asili, Dkt Makalla amewashauri Watanzania kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwani maradhi mengine hayana dalili za moja kwa moja, ila kwa kupima afya huweza kubainika.


“Napenda kupongeza juhudi zinazowekwa na Serikali, kwa kutengeneza miundombinu imara ya kuimarisha sekta ya afya kwa mijini nna vijijini”, alisema Dkt Makalla.


Dkt Makalla yupo nchini Qatar akiendelea kutoa matibabu sambamba na mafunzo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za asili kutoka Norland. 



Kiongozi wa Norland Qatar, Glenda Kissob Salas akifafanua jambo mara baada ya semina fupi ya matumizi sahihi ya tiba lishe za kampuni ya Norland iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Norland Global Tanzania inayojihusisha na tiba lishe yenye makao yake makuu nchini China, Dkt. Moses Makalla




Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Norland Global Tanzania inayojihusisha na tiba lishe yenye makao yake makuu nchini China, Dkt. Moses Makalla (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Hoteli ya Gulf Paradise Sheikh Ali Almarri (wa kwanza kulia) mara baada ya kuwapa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya tibalishe. Wa kwanza kushoto ni Glenda Kissob Salas kionozi wa Norland Qatar.




Mtendaji Mkuu wa Hoteli ya Gulf Paradise Sheikh Ali Almarri (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Norland Global Tanzania inayojihusisha na tiba lishe yenye makao yake makuu nchini China, Dkt. Moses Makalla (kushoto) ofisi wa ajili ya kufanya semina ya matumizi bora ya bidhaa tiba za Norland zinazotibu chanzo cha tatizo, katikati ni Dkt Yusuf Shaban daktari na mshauri wa masuala ya tiba mbadala Qatar.




Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Norland Global Tanzania inayojihusisha na tiba lishe yenye makao yake makuu nchini China, Dkt. Moses Makalla (wa kwanza kushoto) akifanya vipimo vya matibabu kwa Mtendaji Mkuu wa Hoteli ya Gulf Paradise Sheikh Ali Almarri (wa kwanza kulia) ofisini kwake mara baada ya kuwapa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya tibalishe. (wa pili kulia) ni Glenda Kissob Salas kionozi wa Norland Qatar, anayefuata ni Dkt Yusuf Shaban daktari na mshauri wa masuala ya tiba mbadala Qatar.



No comments:

Post a Comment