Tuesday, July 22, 2025

Mgeja anyanyuka kitandani, amvaa Polepole

 


NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI  Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khamis Mgeja amemshukia Balozi Hamphrey Polepole, akimtaka awaombe radhi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kwa kauli aliyoitoa yenye lengo la kukivuruga chama.





Mgeja alisema hayo jana wakati akitoa maoni yake kuhusu kauli ya Polepole ambaye pamoja na mambo.mengine alibeza utaratibu uliotumika kupitisha jina la Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa kiti hicho kupitia CCM.

Katibu huyo wa zamani wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, pia alibeza uteuzi wa Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza na alibeza pia uteuzi wa Dk. Hussein Ally Mwinyi kuwa mgombea pekee wa urais visiwani Zanzibar.


Mgeja ambaye yuko nchini India akipatiwa matibabu alisema Rais Samia,  Dk.Nchimbi Dk Mwinyi ni wagombea halali kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu chama hicho kitapata ushindi wa kimbunga.

"Mimi Khamis  Mgeja ni kada wa CCM, nimewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa Shinyanga na Njumbe  wa NEC taifa, bado nipo nchini India kwa ajili ya matibabu.  Pamoja na kwamba niko kwenye matibabu nimemsikiliza aliyekuwa Polepole akituhumu kwamba kuna mambo hayako sawa  ndani ya chama na Serikali 
"Na hasa kubwa zaidi analalamikia mchakato wa kuwapata wagombea urais kupitia mkutano mkuu wa CCM kwamba  uteuzi wao haukuwa halali na ulinajisiwa kwa kuvunja Katiba na anasema hadi leo hajawapongeza wagombea hao.

" Kwangu mimi naona Polepole haijui vizuri Katiba ya chama  na inawezekana hajawahi kuisoma zaidi ya kufahanu utamaduni na desturi za chama tu jambo ambalo amejidhihirisha kuwa uwezo wake ni mdogo sana wa kuifahamu katiba ya CCM na kuitafasiri kwa usahihi," alisema Mgeja
Aliongeza kuwa uelewa mdogo alionao Polepole katika masuala ya Katiba ndiyo yaliyomfanya ashindwe kutaja ni Ibara au kifungu gani cha Katiba kilichokosewa katika maamuzi ya mkutano mkuu kuteua wagombea urais.
"Polepole ameishia kusema tu desturi na utamaduni wa CCM haukufuatwa na kuzingatiwa huu ni ujinga wa kutoifahamu vizuri Katiba ya chama, napenda kumjulisha yeye na kikundi  chake kilichojificha wafahamu kuwa taratibu zote zlifutwa na maamuzi yalizingatia matakwa ya katiba, wakasome mamlaka ya mkutano mkuu ibara ya  101 na 102 na vifungu vyake vidogo ndipo watakapojua uhalali wa maamuzi ya uteuzi wa wagombea hao,"

Mgeja alisisitiza kuwa uteuzi ulikuwa wa uwazi, majadiliano na mashauriano ya wazee wa chama yaliyotolewa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete yalikuwa bora kabisa.

Mgeja alimkumbusha Polepole miaka michache iliyopita chini ya Rais John Magufuli namna walivyosigina Katiba, kupora mamlaka ya CCM na walikigeuza chama kama kampuni yao binafsi.
" Tulishuhudia demokrasia ikikandamizwa,  Uhuru wa kujieleza ulikandamizwa, vyombo vya habari na  bunge vilikandamizwa watu walizurumiwa fedha zao kwenye Akaunti zao na kubambikiwa kodi ya hovyo, mliharibu mausiano ya nje ya kidiplomasia,  matumizi mabaya ya fedha mpaka mkamfukuza C,A,G kwa kuwaambiwa mnavyofanya hovyo kwenye matumizi ya umma, leo unapata wapi ujasiri wa kukosoa uongozi wa Rais Samia?," alihoji Mgeja

Alimtaka Polepole na genge lake kutambua kuwa kama walikuwa na mgombea wao wa urais imekula kwao, watafute kazi nyigine ya kufanya na CCM itapata ushindi wa kishindo.

Alimsihi Polepole, aende akatubu  kwa upotoshaji na kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania.

 Aidha Mgeja alisema Polepole anafanya kusudi kuwapotosha wananchi kwani anajua matakwa  ya  katiba inavyotaka anapofariki Rais 
 





No comments:

Post a Comment