Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimetangaza rasmi uteuzi wa wakurugenzi wa idara mbalimbali katika ngazi ya taifa, hatua muhimu ya kuimarisha utendaji na maandalizi ya chama kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari, Mawasiliano na Uenezi wa CHAUMMA, John Mrema, aliyesema kuwa uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Katiba ya chama, Ibara ya 73, na kupitishwa na Kamati Kuu ya chama.
“Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma imefanya uteuzi wa wakurugenzi wa idara mbalimbali za chama ngazi ya taifa kwa mujibu wa Katiba ya chama. Hii ni hatua ya kimkakati ya kuimarisha uongozi wa ndani na maandalizi ya kisiasa kwa mustakabali wa nchi,” alisema Mrema.
Walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali ni:
Wakurugenzi wa Idara za Kitaifa
-
Kayumbo Kabutali – Mkurugenzi, Idara ya Bunge, Halmashauri na Serikali za Mitaa.
-
John Mrema – Mkurugenzi, Idara ya Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma; Naibu wake ni Ipyana Samson.
-
Catherine Nyakao Ruge – Mkurugenzi, Idara ya Uchumi, Fedha na Mipango; Naibu wake ni Stewart Kaking’i.
-
Ismail Kangeta – Mkurugenzi, Idara ya Uchaguzi, Kampeni na Organization. Naibu Wakurugenzi:
-
David Chiduo (Organization)
-
Mohamed Pume (Kampeni na Uchaguzi)
-
-
Rahman Hashim Rungwe – Mkurugenzi, Idara ya Mahusiano, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; Naibu wake ni Aisha Madoga.
-
Edward Kinabo – Mkurugenzi, Idara ya Itikadi na Mafunzo; Naibu wake ni Dorice Mpatili.
-
Ester Fulano – Naibu Mkurugenzi, Idara ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu (Mkurugenzi atatangazwa baadaye).
-
Elia Gregory Mahwa – Mkurugenzi, Idara ya Utafiti, Tathmini na Ufuatiliaji; Naibu wake ni Bibiana Benedicto.
-
Prosper Makonya – Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ulinzi na Usalama.
Sekretarieti ya Chama Taifa
-
Julius Gabriel Mwita – Katibu wa Sekretarieti ya Chama Taifa.
-
Reginald Munisi – Mtaalamu wa Mikakati.
-
Khadija Mwago – Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu, Makao Makuu; Msaidizi wake ni Salma Sheriff.
-
Magreth Mlekwa – Mtaalamu wa Dawati la Jinsia, Makao Makuu.
Kwa mujibu wa John Mrema, uteuzi huu unalenga kuleta ufanisi, uwajibikaji na uongozi wa kimaadili unaojibu matarajio ya wananchi.
“Tunahitaji watu makini, waadilifu na wenye dira ya kweli ya ukombozi wa taifa hili. CHAUMMA sasa iko tayari kuingia katika hatua mpya ya kisiasa kwa nguvu mpya na timu yenye uwezo,” alisisitiza Mrema.
Hatua hii inaonesha dhamira ya CHAUMMA ya kujijenga upya kwa mtazamo wa kisera, kiitikadi na kimkakati, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu na kujenga mfumo wa kisiasa unaozingatia haki, usawa na maendeleo ya wananchi wote.

No comments:
Post a Comment