Mwenyekiti wa Chama chaDemokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la uhaini.
Lissu, ambaye anatetewa na jopo la mawakili sita, anakabiliwa pia na mashitaka ya kuchapisha taarifa za uongo kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.
Kwa mujibu wa mashtaka yaliyo wasilishwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, Lissu anadaiwa kutoa matamshi ya uchochezi dhidi ya Serikali, Polisi, na Mahakama akidai kwamba vyombo hivyo havina uhalali wa kusimamia chaguzi kutokana na kuwa "vinateuliwa na Rais na havitendi haki."
Aidha, alishtumiwa kwa kudai kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikumbwa na kasoro kubwa na udanganyifu uliofanywa na vyombo vya dola.
Hata hivyo, Mahakama ya Kisutu ilieleza kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhaini, na hivyo kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 24, 2024.
Lissu alikamatwa siku moja kabla, akiwa mkoani Ruvuma baada ya kumaliza mkutano wa hadhara. Wakati wa kukamatwa, alikuwa akiendeleza kampeni ya CHADEMA inayoitwa โNo Reforms, No Electionโ โ msimamo rasmi wa chama uliopitishwa na Kamati Kuu tarehe 2-3 Desemba 2024.
Msimamo huo unasisitiza kuwa CHADEMA haitashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 iwapo hakutakuwa na mabadiliko ya msingi ya kikatiba, kisheria na kiutendaji katika mfumo wa uchaguzi.
Tukio hilo limeibua taharuki kubwa miongoni mwa wanachama na viongozi wa CHADEMA, ambapo pia inaripotiwa kuwa Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche; Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema; Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini, Aden Mayala; pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, wamekamatwa au kuzuiliwa na Jeshi la Polisi.
Polisi kupitia taarifa yao walitoa onyo kali kwa vyama vya siasa kutotoa kauli zinazodaiwa kuwa za uchochezi au za kuvuruga amani kuelekea uchaguzi ujao.
No comments:
Post a Comment