TANAPA Yafuturisha Watoto Yatima wa Al Furqan Welfare Trust



Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeendesha zoezi la kufuturisha watu mbalimbali wenye uhitaji, likiwemo Kituo cha Watoto Yatima cha Al Furqan Welfare Trust kilichopo mkoani Arusha. 



Hafla hiyo ya iftar ilifanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika jijini Arusha tarehe 27 Machi, 2025, na ilihudhuriwa na viongozi wa dini ya Kiislamu wakiwemo Shekhe Hussein Mwijunje, Shekhe wa Wilaya ya Arusha, Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Musa Juma Kuji, pamoja na watumishi wa TANAPA.



Zoezi hili la kufuturisha lililozungumzia matendo ya sala na huruma katika jamii, limeongeza umoja na mshikamano, na ni sehemu muhimu ya mafundisho ya Kiislamu ambayo yanasisitiza kusaidia wasiojiweza, hasa katika kipindi cha Ramadhani. 





Dini ya Kiislamu inasisitiza umuhimu wa kutoa msaada kwa watu maskini, yatima na wahitaji, na kufuturisha ni njia mojawapo ya kuonyesha upendo, mshikamano na huruma kwa wengine.



Katika kipindi cha Ramadhani, Waislamu wanahimizwa kutoa msaada na kusaidia watu wenye njaa na uhitaji ili kuwaonyesha huruma na upendo. Kufuturisha katika Ramadhani siyo tu kitendo cha kupata thawabu, bali pia ni njia ya kujenga umoja katika jamii na kuleta faraja kwa watu wanaokosa mahitaji muhimu.



Hii ni sehemu ya kujenga maadili mema katika jamii na kueneza amani, kwani kila Muislamu anahimizwa kutenda mema kwa wenzake na kumtukuza Mwenyezi Mungu.

Katika hafla hiyo, watoto yatima wa Al Furqan Welfare Trust walipokea vyakula, mafuta, katoni za maji, soda, na mbuzi mmoja kama sehemu ya zawadi. 


Zawadi hizi ni msaada muhimu kwa watoto hao yatima, ambao wanakosa familia za kuwahudumia, na ni ishara ya msaada wa dhati kutoka kwa TANAPA na viongozi wa dini.


Kufuturisha ni moja ya matendo ya sala katika Ramadhani na ni sehemu ya kutekeleza wajibu wa kijamii unaohusisha kumsaidia jirani, hasa wale walio katika mazingira magumu. 


Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, kitendo cha kutoa ni njia ya kupokea baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ni sehemu ya kujenga jamii yenye huruma, mshikamano na upendo.

0 Comments:

Post a Comment