Moto wa nyika unaoendelea kusababisha madhara makubwa huko Los Angeles umesababisha vifo vya takribani watu 10, huku maafisa wakionya kwamba upepo mkali unaweza kuzidisha moto huo.
Mkuu wa zimamoto katika eneo hilo, alizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC amesema, "Kwa sasa hakuna 'ushahidi wa uhakika' kwamba moto huo ulianzishwa kimakusudi."
Naye Mkuu wa Polisi wa Kaunti ya Los Angeles, Robert Luna, alisema, "Si salama kufikia maeneo mengi yaliyoathiriwa," na kuongeza kuwa, "Tunatarajia idadi ya vifo kuongezeka."
Kwa mujibu wa tovuti inayofuatilia kukatika kwa umeme nchini Marekani, takriban nyumba na majengo ya kibiashara 100,000 hayana umeme huko Los Angeles, huku zaidi ya watu 100,000 wakiwa wamelazimika kuhamishwa kutoka maeneo yaliyoathiriwa na moto huo.
Wakati huo huo mwana wa kiume wa Rais, Trump yaani Donald Trump Junior, ameuhusisha moto wa California na msaada wa Marekani kwa Ukraine na kumtaja Biden kuwa anabeba dhima katika uwanja huo.
Mtoto huyo wa Trump amechapisha vichwa vya habari kwenye mitandao ya kijamii ambavyo vinaonyesha namna Idara ya Zimamoto ya Los Angeles huko nyuma ilivyotoa vifaa vyake ili kuisaidia Ukraine.
Akisisitiza kuwa usimamizi mbaya wa Serikali ya Shirikisho ya Marekani katika kushughulikia majanga ya kimaumbile kama vile Kimbunga cha Katrina kilichoikumba nchi hiyo mwaka 2005 katika majimbo kadhaa ya kusini mwa nchi, na vilevile moto wa miaka iliyopita huko California na serikali kushindwa kuwasaidia waathiriwa wa maafa hayo ni moja ya masuala ambayo yamedhihirika wazi zaidi. Wakati huo huo serikali hii ya Marekani, ambayo haiwezi kukabiliana na migogoro na matatizo yake ya ndani, inadai kushughulikia na kuipatia ufumbuzi migogoro ya kikanda na kimataifa.
No comments:
Post a Comment