Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amemuonya Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo (CCM), kuacha tabia ya kutafuta umaarufu kwa kutangaza matatizo ya wananchi mbele ya jamii, badala yake amemshauri ahudhurie vikao na kushirikiana na wadau wengine kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Makonda aliyasema haya wakati akizungumza na Gambo katika ziara ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini-Olemringaringa-Sambasha yenye urefu wa kilomita 18, katika eneo la Ilboru, Arusha, leo Jumatatu, Januari 6, 2025.
"Baadhi ya matatizo ya wananchi yanajadiliwa kwenye vikao lakini Gambo anakuwa hahudhurii. Hii ni tabia ya kutaka umaarufu bila ya kutoa mchango wa maana katika kutatua changamoto hizo. Kama kweli anataka kusaidia, aahudhurie vikao na kujadili yale mambo ambayo yamekubaliwa na wadau wote," alisema Makonda.
Aliongeza kuwa, "Hii ni fursa nzuri kwa viongozi wote kushirikiana katika kutatua changamoto za wananchi. Ni muhimu kuwa na ushirikiano wa dhati badala ya kutafuta umaarufu kwa maneno ya nje."
Ziara hiyo ya Waziri Ulega ilikuwa ni sehemu ya shughuli za ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa wa Arusha.
0 Comments:
Post a Comment