Samia Atangaza wajumbe wa Tume Mbili Kuchunguza Masuala ya Ardhi na Uhamaji katika Hifadhi ya Ngorongoro

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza wajumbe wa Tume mbili zilizoundwa na Serikali ili kufuatilia na kufanya tathmini kuhusu masuala muhimu yanayohusu Hifadhi ya Ngorongoro. 


Tume ya Kwanza itafanya tathmini kuhusu mgogoro wa ardhi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, ambapo masuala ya ardhi yamekuwa yakiibua malalamiko kutoka kwa wakazi wa eneo hilo. 


Tume ya Pili itatathmini utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari wa wakazi wa Hifadhi ya Ngorongoro, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhamasisha maendeleo ya jamii katika eneo hilo.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro na kumteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dkt. Gerald Ndika, kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo. Wajumbe wa Tume hiyo ni:

  1. Philemon Luhanjo - Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu
  2. Zakia Hamdani Meghji - Aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii
  3. Jaji George Mcheche Masaju - Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria
  4. Dkt. Richard Muyungi - Mshauri wa Rais, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  5. Balozi Salome Sijaona - Balozi na Katibu Mkuu Mstaafu
  6. Prof. Wilbard Kombe - Profesa wa Chuo Kikuu Ardhi
  7. Prof. Emmanuel Luoga - Profesa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
  8. Mollel James Moringe - Diwani na Katibu wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro
  9. Moi Aprakwa Sikorei - Diwani na Mkazi wa Ngorongoro


Kwa upande mwingine, Rais Samia ameunda Tume ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kumteua Mhandisi Musa Iyombe, Katibu Mkuu Mstaafu, kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo. Wajumbe wa Tume hii ni:

  1. Sihaba Nkinga - Katibu Mkuu Mstaafu
  2. Alphayo Kidata - Mshauri wa Rais, Uwezeshaji Biashara na Masuala ya Kodi
  3. Balozi Valentino Mlowola - Balozi Mstaafu na aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
  4. Balozi Mohamed Mtonga - Balozi Mstaafu na aliwahi kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali
  5. Balozi George Madafa - Balozi Mstaafu
  6. Haruna Masebu - Aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba (NHO)
  7. Edward Maura Nduleti - Diwani na Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro
  8. Rehema Moisare - Mwalimu na Mkazi wa Ngorongoro

Hatua hii ni muhimu kwa kuangalia masuala ya ardhi na uhamaji katika Hifadhi ya Ngorongoro, na ina lengo la kutatua migogoro na kukuza maendeleo endelevu kwa jamii zinazohusika.

0 Comments:

Post a Comment