Serikali imetolea majibu maswali yaliyoulizwa bungeni kuhusu upungufu wa walimu katika shule za msingi na sekondari katika Jimbo la Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro.
Swali hili lilikuwa limeulizwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Patrick Ndakidemi, akihoji mipango ya Serikali kuongeza idadi ya walimu katika shule hizo ambazo zinakabiliwa na upungufu mkubwa.
Katika majibu yake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Athuman Katimba, alieleza kuwa Serikali inaendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuboresha upatikanaji wa walimu kwa ajili ya shule za msingi na sekondari katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Jimbo la Moshi Vijijini.
Alisema kuwa serikali imeongeza idadi ya walimu kupitia mpango wa ajira mpya na inaendelea kufanya tathmini ya mahitaji ya walimu ili kuhakikisha kwamba shule zote zinazopokea wanafunzi kwa idadi kubwa zinapata walimu wa kutosha.
Zainab aliongeza kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa elimu, Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa maeneo husika ili kuhakikisha kuwa changamoto za upungufu wa walimu zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
0 Comments:
Post a Comment