Sunday, October 20, 2024

TAMASHA LA VIJANA NA UONGOZI HIMO LAFANA. MAMIA YA VIJANA WAJITOKEZA CDE SHIRIMA ATAKA KAZI ZA RAIS ZISEMWE BILA KIFICHO

 




Na Gift Mongi

Moshi


Ni hatua ya matumaini hivyo ndiyo ilivyojitokeza kwa vijana mbalimbali waliojitokeza katika viwanja vya mji mdogo wa Himo uliopo katika Halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro.



Ni tukio la kipekee lililoandaliwa na mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirika


Ndio!ndio!vijana na uongozi ilikuwa ni kauli mbiu katika tamasha hilo lililosheheni mamia ya vijana kutoka katika pande mbalimbali za wilaya na hata nje.


Je ni KWANINI VIJANA?

Mmoja wa washiriki ambaye hakutaka kuna lake lionekane katika vyombo vya habari alisema kuwa vijana ndio chimbuko la maendeleo 


"Sisi kama vijana hatukuja hapa kupoteza muda ila ni ishara kuwa sisi ni viongozi wajao na kipekee tunashukuru 

mwenyekiti wetu Cde Yuvenail  Shirima kwa kazi huu kubwa aliyoifanya


Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM Yuvenail Shirima aliwataka vijana kujitoa kwa hali na mali katika kusema mazuri yanayofanywa na serikali badala ya kukaa kimya.


"Tumekutana hapa leo Himo yapo mengi yanafanywa na mwenyekiti wetu na rais Dkt Samia Suluhu Hasan ebu kayasemeni watu wayajue'alisema

No comments:

Post a Comment