Mnyika Atoa Wito Kwa Watanzania Kujitokeza Kwa Wingi Kujiandikisha Upya

 


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, ametoa wito kwa Watanzania wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura litakalofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024 katika vituo vya Mtaa, Kijiji au Kitongoji. 


Akizungumza kuhusu umuhimu wa zoezi hilo, Mnyika alisisitiza kuwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anatakiwa kujiandikisha upya, hata kama tayari ana kadi ya kupigia kura. 


"Jiandikishe ili uweze kutumia haki yako ya kupiga kura ifikapo tarehe 27 Novemba 2024," alisema Mnyika, akiongeza kuwa vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi kila siku ndani ya kipindi hicho.


Zoezi hili ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi ujao, na lina lengo la kuhakikisha kila mpiga kura anakuwa kwenye daftari la wakazi la eneo lake, ili kuweza kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.

0 Comments:

Post a Comment