Friday, October 25, 2024

HOSPITALI YA GEMSA POLYCLINIC YAANZISHA KAMBI YA MATIBABU BURE SIKU TATU MKOANI ARUSHA



Happy Lazaro,Arusha .


Hospitali ya Gemsa Polyclinic iliyopo mkoani Arusha imeanzisha kambi ya siku tatu ya upimaji na utoaji elimu wa saratani ya matiti na tezi  dume bure Arusha wananchi  wa mkoa wa Arusha kuanzia oktoba 24 hadi 26 .



Akizungumza  na waandishi wa habari kwenye kambi hiyo,Daktari wa magonjwa yote kutoka hospitali hiyo,Dokta  Kelvin Kimal amesema kuwa , huduma  hizo zote  zinatolewa bure lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya saratani ya matiti na tezi dume kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kwani bado ni changamoto. 



Dokta Kimal amesema kuwa, upimaji huo unaenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi hao juu ya magonjwa hayo  na kuweza kupata elimu namna ya kuzigundua dalili mapema  kwani bado elimu ni changamoto. 



Aidha Dokta Kimal amefafanua kuwa, changamoto iliyopo ni wananchi wengi kufika kupata matibabu ya magonjwa hayo hali  ikiwa imekuwa mbaya zaidi jambo ambalo linakuwa  ni changamoto  katika kupata matibabu ,hivyo  kupitia kambi hiyo wanaweza kupatiwa elimu namna ya kuzijua  dalili mapema  na kuweza kuwahi kupata huduma kabla tatizo halijawa  kubwa zaidi.



"Tumeamua kuweka kambi hii kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na kuweza kupatiwa vipimo vya awali na kuweza kupatiwa elimu namna ya kuweza kujipima wenyewe pia  "amesema .


Aidha amefafanua zaidi kuwa,vipimo hivyo vinapimwa kwa kutumia kifaa cha ultra  sound na kuweza kuonana na madaktari na kuweza kushauriwa namna ya kufanya endapo watagundua kuwepo kwa dalili hizo .


Aidha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo ya huduma bure na matibabu kwani kutokea ni mara chache sana .



Kwa upande wake  ,Daktari wa magonjwa yote ,Amne Munir Saggaf amesema kuwa, kambi kama hiyo walishafanya miaka miwili iliyopita  ambapo mwitikio ulikuwa mkubwa sana wa wananchi ambapo wanatamani waifanye  kila mwaka kwani uhitaji ni mkubwa sana .


Saggaf amefafanua kuwa,wamejitahidi kuboresha huduma hizo kwa mwaka huu  lengo likiwa ni kuona  wananchi wengi wa Arusha wanapata  huduma hiyo na kuweza kupata matibabu pia. 


"Katika kambi hii ya siku tatu tunatarajia kufikia wananchi Mia tano ambao tunatarajia watakuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao kwa kutoa elimu ambayo tutakuwa tumewapatia ili waweze kuzijua  dalili za magonjwa hayo  na kuweza kupata matibabu mapema. "amesema dokta Saggaf.


Mmoja wa wananchi waliopata  huduma hospitali hapo,Januari  Chami kutoka Sombetini  amesema kuwa amefurahia  huduma hiyo kwani unapata  fursa ya kupata elimu kuhusu magonjwa hayo na dalili zake ili kuweza kuwahi matibabu  mapema .


"Kwa kweli nimefurahi sana nimeweza  kupima tezi dume na figo  na nimekutwa  sina  shida yoyote nawaomba wananchi wa Arusha wajitokeze  kwa wingi kuchangamkia fursa hii  inayotolewa  bure hapa hospitali ya Gemsa kwani ni adimu  sana kupatikani .



No comments:

Post a Comment