Saturday, October 26, 2024

CHADEMA Yakanusha Taarifa za Kujitoa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

 



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha vikali taarifa zinazosambaa kwenye CHADEMA Yapinga Taarifa za Kujitoa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya kijamii zikidai kuwa chama hicho kimejitoa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.


Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema,  Oktoba 25 , 2024, imeeleza kuwa video inayosambaa ikidai CHADEMA imejiondoa kwenye uchaguzi huo ni ya "uongo na uzushi," na imewataka wananchi kupuuza taarifa hizo.


_"Tunapenda kutoa taarifa kuwa picha mjongeo inayosambaa mitandaoni yenye maudhui kuwa CHADEMA imejitoa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 ni ya uongo na uzushi, hivyo ipuuzwe,"_ alisema Mrema.



CHADEMA imesisitiza kuwa bado ipo kwenye mchakato wa uchaguzi na haina mpango wowote wa kujitoa. Mrema alitoa wito kwa wanachama wa chama hicho walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo kujitokeza mapema kesho, tarehe 26 Oktoba, 2024, kuchukua fomu za kugombea.


_"Tunawahimiza wanachama wetu walioteuliwa nchi nzima kesho tarehe 26 Oktoba, 2024 wajitokeze mapema kwenda kuchukua fomu za Serikali za kugombea nafasi mbalimbali walizoteuliwa na Chama,"_ Mrema alisisitiza.



No comments:

Post a Comment