Monday, August 19, 2024

Wanne, Wakiwemo Wanajeshi Wawili, Waburuzwa Kortini kwa Kubaka na Kulawiti Binti wa Yombo Dovya




Watu wanne, wakiwemo wanajeshi wawili, wamefikishwa wakikabiliwa na makosa ya kubaka kwa kundi na kulawiti. 

Watu hao kwenye kesi hiyo yenye kufuatiliwa na wengi wamefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma leo, Agosti 19, 2024, 

Washtakiwa hao ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, askari wa JWTZ, Amin Lord Lema, Nickson Idala Jackson, na C.1693 Praygod Edwin Mushi, askari Magereza.


Wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Zabibu Mpangula ambapo kosa la kwanza wanakabiliwa nalo ni kubaka kwa kundi, na la pili ni kumuingilia kinyume cha maumbile binti huyo.


Kulingana na taarifa kutoka kwa Renatus Mkude, Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano kuanzia leo hadi Ijumaa, Agosti 23, 2024.


 Watuhumiwa wamekana makosa yao na wamepelekwa mahabusu gerezani na mahakama itahakikisha usalama wa binti aliyepata madhila, huku jina lake likihifadhiwa kulingana na sheria. 

No comments:

Post a Comment