Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Amos Lwiza (54), mkazi wa Tegeta Wazo wilaya ya Kinondoni, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mitandaoni. Taarifa hizo zilidai kuwa binti mkazi wa Yombo Dovya, ambaye video zake zilisambaa mitandaoni akibakwa na kulawitiwa na vijana watano, amekutwa tayari amefariki dunia.
Kamanda Muliro, akizungumza leo Agosti 7, 2024, ameeleza kuwa binti huyo bado yupo hai na hajafa, kama ambavyo taarifa za uongo zimekuwa zikisambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii. Aidha, uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
Kamanda Muliro pia amesema kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini na kuwachukulia hatua waliohusika kwenye tukio la ubakaji na ulawiti.
0 Comments:
Post a Comment