Monday, August 12, 2024

Polisi Mbeya Wamkamata Mbowe na Pambalu Uwanja wa Ndege Songwe

 



Polisi Mkoani Mbeya wamemkamata Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), John Pambalu, muda mfupi baada ya wawili hao kuwasili uwanja wa ndege wa Songwe leo, Agosti 12, 2024.


Mbowe alikamatwa alipowasili uwanja wa ndege wa Songwe kwa lengo la kufuatilia hatima ya viongozi wa CHADEMA waliokamatwa jana, Agosti 11, 2024, katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyasa. Viongozi waliokamatwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara, Tundu Lissu; Katibu Mkuu, John Mnyika; na Mwenyekiti wa Kanda, Joseph Mbilinyi (SUGU).


Lissu, Mnyika, na Sugu waliwasili Mbeya jana ili kuungana na vijana wa CHADEMA kupitia BAVICHA kwa maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani iliyokuwa imeandaliwa leo Jijini Mbeya, lakini walikamatwa kabla ya shughuli kuanza.


John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje - CHADEMA, amethibitisha kukamatwa kwa Mbowe na Pambalu, akisema, “Mbowe na John Pambalu walipofika uwanja wa ndege wa Songwe leo wamekamatwa na Jeshi la Polisi, ukamataji huu umeongozwa na RPC wa Mbeya. Tutaendelea kuwapa taarifa kadiri tunavyozipata.”

No comments:

Post a Comment