WAGOMBEA wa nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), jana wameshiriki mdahalo wa kunadi sera zao wengi wakiwa na shauku ya kuimarisha heshima ya mawakili nchini huku mgombea Boniface Mwabukusi akionekana kung'aa zaidi.
Agosti mosi hadi 3, mwaka huu, chama hicho kinatarajia kufanya mkutano mkuu wake ambao moja ya majukumu ni kumchagua Rais wa TLS.
Wagombea wanaowania nafasi hiyo ni pamoja na Wakili Sweetbert Nkuba, Paul Kaunda, Revocatus Kuuli, Emmanuel Muga, Ibrahim Bendera na Boniface Mwabukusi.
Katika mdahalo huo ulioandaliwa na Star TV, wagombea hao wamenadi sera zao ambapo Mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Mwabukuzi alisema anataka nafasi hiyo ili kuleta mageuzi ambayo kwa muda mrefu yameshindikana ikiwemo kupambana na mafisadi kwenye chama hicho na nje ya chama.
Alisema TLS kwa muda mrefu imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kusaidia wanachama kutokana na watu wanaochaguliwa kuiogopa serikali hali ambayo iliwafanya washindwe kusimamia misingi ya kuanzishwa kwa TLS.
"Mageuzi ni muhimu ili TLS irejee kwenye misingi yake ya kusaidia na kuwalinda wanachama wake," alisema Mwabukuzi. Alisisitiza kuwa ni wakati wa chama hicho kuchukua hatua kali dhidi ya ufisadi na kuhakikisha haki inatendeka kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla.
Mwabukuzi aliahidi kuwa endapo atachaguliwa, atahakikisha TLS inarudi kwenye mstari wa kutetea haki za wanachama na kupambana na vitendo vya ufisadi. "Tunahitaji viongozi jasiri ambao hawataogopa kusimama imara dhidi ya uonevu na ufisadi," aliongeza.
Alisema kuwa TLS inahitaji mageuzi ya haraka ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuleta mabadiliko chanya kwa wanachama na sekta ya sheria kwa ujumla. "Ni wakati wa TLS kuwa taasisi inayojali maslahi ya wanachama wake na jamii kwa ujumla," alisema Mwabukuzi.
Mwabukuzi alitoa wito kwa wanachama wa TLS kumchagua ili aweze kuleta mabadiliko hayo na kuhakikisha chama hicho kinarejea kwenye misingi yake ya msingi. Aliahidi kushirikiana na wanachama wote kuhakikisha kuwa TLS inafanya kazi kwa uwazi, uadilifu, na kwa manufaa ya wote.
"Mageuzi haya hayatawezekana bila ushirikiano wenu. Ni lazima tuwe na mshikamano ili kupambana na changamoto zinazotukabili na kuhakikisha kuwa TLS inasimama imara kama taasisi inayoongoza kwa haki na uadilifu," alisema Mwabukuzi.
Mwabukuzi alimalizia kwa kusema kuwa ni wakati wa mabadiliko ndani ya TLS na kwamba yeye yupo tayari kuongoza mapambano hayo kwa nia ya kuleta haki na usawa ndani ya chama na katika jamii kwa ujumla.
Mgombea Wakili Home
habari
KAMPENI UCHAGUZI TLS ZAPAMBA MOTO
Sunday, July 28, 2024
Picha zikiwaonesha wagombea Mbalimbali wanaowania nafasi ya Chama Cha Wanasheria Tanzania (TLS)
Na Mwandishi Wetu
WAGOMBEA wa nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), jana wameshiriki mdahalo wa kunadi sera zao huku wengi wakiwa na shauku ya kuimarisha heshima ya mawakili nchini.
Agosti mosi hadi 3, mwaka huu, chama hicho kinatarajia kufanya mkutano mkuu wake ambao moja ya majukumu ni kumchagua Rais wa TLS.
Wagombea wanaowania nafasi hiyo ni Wakili Sweetbert Nkuba, Paul Kaunda, Revocatus Kuuli, Emmanuel Muga, Ibrahim Bendera na Boniface Mwabukusi.
Katika mdahalo huo ulioandaliwa na moja ya chombo cha habari cha televisheni nchini, wagombea hao wamenadi sera zao ambapo Mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Sweetbert Nkuba, alisema anauzoefu wa muda mrefu wa uongozi katika ngazi mbalimbali na kuomba achaguliwe kwenye nafasi hiyo ili afanikishe vipaumbele vitano ikiwemo kuwaunganisha wanachama wa TLS na kuhakikisha maslahi ya kiuchumi ya wanachama wa chama hicho yanazingatiwa.
Alisema atahakikisha inatungwa sera ya jinsia kwa TLS na atalinda na kuitetea taaluma ya uwakili kwa wivu mkubwa.
Wakili Nkuba alisema anaamini uimarishaji wa miundombinu ya kisheria na kiteknolojia ndani ya TLS utawezesha huduma bora kwa wanachama na jamii kwa ujumla kwa kuongeza uwekezaji katika mifumo ya kidijitali ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na huduma za kisheria.
Pia alisema akichaguliwa atazingatia masuala ya mafunzo na utaalamu ili kuhakikisha kuwa wanasheria wana ujuzi wa kisasa na uwezo wa kushindana kimataifa.
Alisema sera yake ni ushawishi na utetezi kwa kuhakikisha TLS inakuwa na sauti yenye nguvu katika masuala ya kitaifa na kimataifa yanayohusu sheria na haki.
“ Hii itajumuisha:Kuanzisha mikakati ya ushawishi kwa serikali na bunge ili kuboresha mfumo wa sheria nchini, kutoa msaada wa kisheria kwa jamii, hususan makundi yenye uhitaji maalum,”alisema.
Kadhalika, alisema atazingatia uwajibikaji kwa kusimamia kwa uwazi na uwajibikaji katika shughuli zote za TLS ili kujenga imani kwa wanachama na wadau wengine ikiwamo kuboresha mifumo ya ukaguzi wa ndani na nje ili kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali za TLS na kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wanachama kuhusu shughuli na matumizi ya fedha za TLS.
“Nimedhamiria kujenga mahusiano imara kwa wadau mbalimbali, ikiwamo serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na taasisi za kimataifa. Hii itajumuisha: Kuanzisha na kudumisha ushirikiano na mashirika ya kimataifa ya kisheria kwa manufaa ya wanachama wa TLS, Kushirikiana na vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu katika kutoa elimu ya sheria na mafunzo ya vitendo,”alisema.
Kadhalika, alisema atakuza uongozi na ushirikishwaji kwa kuhakikisha wanachama wa TLS wanashiriki kikamilifu katika maamuzi na uongozi wa chama.
“Nitaanzisha mfuko wa malipo ya ada yam waka kwa unafuu, kuanzisha na kusimamia vituo vya malezi kwa mawakili wapya, upatikanaji wa bima ya afya kwa utaratibu wa kulipa kidogo kidogo,”alisema.
Naye, Mgombea Wakili Paul Kaunda alisema anataka kuwalinda na kuwatetea mawakili wachanga kwa kuwaongezea thamani na heshima ikiwamo kuja na Wakili APP ambayo itasaidia mawakili kupata wateja kwa urahisi na kupata malipo stahiki kwa mujibu wa sheria ya gharama za mawakili itakuwa kama UBA.
Alisema atamshauri na kumshirikisha mwanasheria mkuu wa serikali kutunga kanuni zitakazotulinda mawakili na kuwaheshimisha mawakili wanapofanya majukumu wao wakiwa Mahakamani, polisi na vyombo vingine.
Pia alisema atamshauri na kumshirikisha Jaji Mkuu wa Tanzania aone umuhimu wa kuanzisha Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Teknolojia, ili kuiandaa mahakama ambayo itahusika na mambo yaliyojitokeza kwenye teknolojia ikiwamo Akili Mnemba.
Mgombea Wakili Ibrahim Bendera alisema amedhamiria kuwaunganisha mawakili vijana na wale wa muda mrefu ili kuwasaidia kusimamia kuwajenga kitaaluma na kupata wateja.
“Kuna matatizo kwenye chama chetu mtu anakuuliza ni chama gani cha siasa, hakuna mwanasheria ambaye sio mwanasiasa tunachoangalia ni vigezo vya kitaaluma, mimi nikichaguliwa ndani ya chama sitaleta mambo ya huyu ni chama gani cha siasa tutafuata msingi wa Martin Luther,”alisema.
Mgombea mwingine ambaye ni Wakili Revocatus Kuuli, alisema akichaguliwa atazingatia masuala ya utawala wa sheria ikiwamo mgawanyo wa madaraka kwa dola, uhuru wa kutoa maoni ili kusaidia nchi bila vitisho na demokrasia kuwa na uchaguzi huru na haki.
Aliomba achaguliwe kwa kuwa amekomaa kuwa kiongozi mwenye msimamo na atakayesimamia uimara wa chama.
Mgombea Wakili Emmanuel Muga, anasema akichaguliwa atatengeneza mpango mkakati unaoendana na wakati wa sasa na atasimamia mafunzo na maadili ya Mawakili.
Alisema ataimarisha utawala kwa kutengeneza kamati zenye uwezo wa kufanya kazi na kuifanya TLS kufuata taratibu za kisheria na sio kuendesha mambo yake kiholela.
No comments:
Post a Comment