Kauli ya Nnauye yaonekana Kukinzana na Ahadi za Mageuzi ya Kisiasa ya Rais Samia



Miaka sita iliyofuata ya Rais John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo, iligubikwa na kile kilichoelezwa kuwa ukandamizaji wa haki za msingi za siasa na demokrasia. Lakini baada ya kuchukua madaraka, mrithi wake Rais Samia Suluhu Hassan, aliahidi kufanya mageuzi ya kisiasa na kidemokrasia pia.


“Ninawaahidi mageuzi zaidi ya kisiasa ili kujenga taifa letu jipya kupitia siasa za ushindani,” alisema Rais Samia alipokuwa akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani yaliyoandaliwa na Baraza la Wanawake Chadema.


Mwaka mmoja kabla, Rais Samia alitambulisha falsafa aliyoiita 4Rs, yaani Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reforms (Mabadiliko), na Rebuilding (Ujenzi Mpya), zifanyike kama dira ya alichosema kuwa ni dhamira yake ya kuleta mageuzi ya kisiasa nchini Tanzania.


Mapema Februari mwaka huu, Bunge lilibadilisha sheria tatu za uchaguzi – vyote vikiwa ishara ya mageuzi. Pamoja na kukiuka misingi ya kimedokrasia.



Hivyo kauli aliyoitoa Nnauye mwanzoni mwa wiki hii imeonekana kukiuka ahadi hiyo ya Rais Samia kufanya mageuzi ya kisiasa na demokrasia.

ameomba radhi akidao kauli yake ni utani baada ya mjadala kuibuka kufuatia kauli aliyoitoa katika kipande cha video kilichosambaa katika mitandao ya kijami kuhusu namna ushindi unaweza kupatikana katika uchaguzi.


"Matokeo ya kura si lazima yawe yale ya kwenye box. Inategemea nani anayehesabu na kutangaza. Na kuna mbinu nyingi, kuna halali, kuna nusu halali na kuna haramu. Na zote zinaweza kutumika, ilimaradi tu ukishamaliza, unamwambia Mwenyezi Mungu nisamehe pale nilipokosea” Nnauye aliwaambia wafanyabiashara katika soko la Kashai mjini Bukoba mkoani Kagera.


Nnauye alishangiliwa na wafanyabiashara hao, lakini katika mitandao ya kijamii wengi walimpinga na kumkosoa kwa kutoa kauli hiyo.

Mchambuzi wa siasa Ezekiel Mollel akiongelea amesema, namna pekee ya kurejesha imani kwa wananchi kwamba hiyo kauli kweli ilikuwa utani, itategemea na mchakato wa uchaguzi utakavyokwenda na jinsi vyombo husika vitakavyosimamia uchaguzi huo.


“Vitu vikienda kushoto, au pakiwa na hitilafu ya namna yoyote ile, wadau watarejea na kusema ‘hili limeshasemwa’. Alichofanya ni jambo zuri, muungwana akikosea shurti aombe radhi. Lakini namna pekee ya kurudisha imani kwa wananchi itaonekana kwenye mchakato wa uchaguzi na si kwenye hii kauli ya kuomba radhi,” alisema Mollel.



0 Comments:

Post a Comment