Thursday, June 27, 2024

KiliMedAir YAJA NA HUDUMA YA UOKOAJI KWA HELIKOPTA

  KiliMedAir  YAJA NA HUDUMA YA UOKOAJI KWA HELIKOPTA


Happy Lazaro,Arusha.


Kampuni ya uokoaji ya KiliMedAir Aviation iliyopo mkoani Kilimanjaro  imeanzisha huduma ya uokoaji wa haraka kwa njia ya helikopta ili kuweza kuokoa muda na kufika eneo la tukio haraka kabla madhara yoyote hayajatokea. 



Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa maswala ya afya katika kampuni hiyo,Dk .Hussein Abradha wakati akizungumza kwenye kambi ya madaktari bingwa wanaotoa huduma za matibabu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo  mkoani Arusha .


"Sisi tumeshiriki  katika kambi hii lengo la kutoa elimu kwa wadau na wananchi ili waweze kuelewa kampuni yetu  na ufahamu shughuli  tunazofanya katika kuwahudumia wananchi kwa wakati na kuokoa muda kwa kutumia helikopta "amesema.


Dk.Hussein amesema kuwa,kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma ya uokoaji kwa watu waliopata dharura  katika maeneo mbalimbali ikiwemo hifadhi na hata maporini kwani helikopta  hiyo ina uwezo wa kupenya  popote kwa wakati na muda muafaka .


Amesema kuwa,wamekuwa wakitoa huduma hiyo ndani ya hifadhi ya Tanapa kwa kuwahudumia watalii na hata wageni mbalimbali wanaopatwa  na changamoto zozote wanapokuwa maeneo ya hifadhi na hata mlimani ambapo wamekuwa wakifika kwa wakati kwa ajili ya kuwawahisha kupata huduma ya haraka  sehemu husika.


"ndani ya helikopta hiyo kunakuwepo na daktari  kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza pindi wanapomkuta  mteja  kapata  changamoto yoyote kabla ya kumwahisha  hospitali kupata huduma zingine na tumejikita  zaidi  kwenye maeneo ya porini milimani pamoja na mbugani katika kuhudumia wageni pamoja na watalii wa nje "amesema Dk.Hussein.


Ameongeza kuwa, ambulance hiyo ya helikopta imekuwa ikitoa huduma kwa wagonjwa wanaokumbana na changamoto  mbalimbali wakiwa maeneo ya hifadhi,porini  na hata mbugani kwani ina uwezo wa kutua  popote .


Amesema kuwa, mbali na huduma hiyo wamekuwa wakitoa huduma zingine za anga ikiwemo za kukodishwa kwa ajili ya kuhudumia watalii  kulingana na mahitaji ya mteja anavyotaka. 


Aidha ametoa wito kwa wadau mbalimbali wakiwemo hospitali mbalimbali  kuitumia kampuni hiyo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za haraka  na kwa muda muafaka .


Nao baadhi ya wananchi ,Selina Mohamed wamepongeza utoaji wa huduma hiyo ya matibabu kwani inaleta manufaa makubwa sana kwao na kuokoa gharama badala ya kwenda kufuata huduma hiyo mbali wanaweza kuipata  hapa hapa kwa haraka na muda muafaka .


"Tunaomba muda zaidi uongezwe  kwani wiki moja haitoshi kabisa kutokana na kuwa wananchi wanaohitaji huduma hiyo ni wengi na hivyo wiki moja haitoshi kabisa kuwafikia wananchi wote."wamesema wananchi hao.





No comments:

Post a Comment