Saturday, June 29, 2024

Biden Ajibu Shutuma Kuhusu Umri Wake, Aahidi Ushindi Katika Uchaguzi wa Novemba

  Biden Ajibu Shutuma Kuhusu Umri Wake, Aahidi Ushindi Katika Uchaguzi wa Novemba



Rais wa Marekani Joe Biden amejibu shutuma zinazotolewa kuhusu umri wake, akiwaahidi wafuasi wake kuwa atashinda tena uchaguzi wa Novemba licha ya wasiwasi uliotokana na utendaji wake katika mdahalo wa urais.


"Najua mimi si kijana, kusema kweli," alisema katika mkutano huko North Carolina siku ya Ijumaa, siku moja baada ya kupata changamoto katika mjadala wa televisheni dhidi ya mpinzani wake wa Republican, Donald Trump. "Sitembei kirahisi kama nilivyokuwa zamani... Sijadili kama nilivyokuwa nikijadili," alikiri. "Lakini ninachojua kwa hakika ni jinsi ya kufanya kazi hii."


Bw Biden, mwenye umri wa miaka 81, alisema anaamini kwa "moyo mmoja" kwamba anaweza kuhudumu muhula mwingine, huku umati wa watu waliokuwa wakishangilia mjini Raleigh wakisema kwa sauti "miaka minne zaidi".


Wakati huo huo, Trump alifanya mkutano huko Virginia saa chache baadaye, ambapo alisifia "ushindi wake mkubwa" katika mjadala huo. CNN iliripoti kuwa mjadala huo ulitazamwa na watu milioni 48 kwenye televisheni na mamilioni zaidi mtandaoni.


"Tatizo la Joe Biden sio umri wake," alisema Trump mwenye umri wa miaka 78. "Ni uwezo wake. Hana uwezo kabisa." Rais huyo wa zamani alisema haamini uvumi kwamba Bw Biden angejiondoa katika kinyang'anyiro hicho, akisisitiza kwamba "anafanya vyema zaidi katika uchaguzi" kuliko wagombea wengine wa Democratic, akiwemo Gavana wa California Gavin Newsom na Makamu wa Rais Kamala Harris.

No comments:

Post a Comment