Sunday, June 5, 2022

WATATU WAFA KWA AJALI UDOM


WANACHUO  watatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,(Udom) wamefariki na wengine watano kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana jioni kwenye moja ya barabara zilizopo ndani chuoni hicho.

 Akizungumza leo Jumapili Juni 5, 2022 na Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Beatrece Baltazar amesema ajali hiyo imetokea jana saa 2.00 usiku.

Amewataja waliofariki kuwa ni Hana Meshack, Zira Mpenda, Mpeli Mahenge.

Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Fortunata Kingazi, Fibi Julius, Sifa Shora, Enica William na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Furahina.

Beatrice amesema majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na hali zao zinaendelea vizuri.

Taarifa zinasema wanafunzi hao walikuwa wanatoka katika mahafali ya dini yaliyokuwa yakifanyika chuoni hapo.

No comments:

Post a Comment