Tuesday, June 14, 2022

WABUNGE WANAWAKE WA MABUNGE YA AFRIKA KUKUTANA ARUSHA


WABUNGE Wanawake kutoka mabunge ya kikanda barani Afrika kukutana jijini Arusha  kujadili changamoto, mafanikio na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwawezesha kuwahamasisha  wanawake wengine kushiriki kwenye siasa ili kuweza kufikia uwiano wa 50/50 kwenye uongozi.


Aidha, Spika wa Bunge la  Tanzania, DKT. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa siku tatu uliondaliwa na taasisi ya kimataifa ya Uongozi demokrasia usawa wa kijinsia ya IDEA , (International IDEA).





Katibu wa Umoja wa wabunge Wanawake wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA) Fatuma Ndangiza amewaeleza waandishi wa habari leo, Juni 14, 2022 kuwa mbali ya wabunge pia mkutano huo utajumisha makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo waandishi wa habari.


 


Amesema pamoja na changamoto pia watapeana uzoefu utakaosaidia kuongeza wigo wa viongozi wanawake ili kufikia malengo ya azimio la Beijing la kufikia walau asilimia 30 ambapo kwa Sasa imefikiwa asilimia 25 pekee.



Katibu huyo wa wabunge wanawake wa EALA,  ameabainisha kuwa washiriki wa Mkutano huo ni pamoja na wabunge kutoka wa mabunge ya nchi mbalimbali xa Afrika pamoja na kikanda ikiwemo EALA SADC ECOWAS COMESA , Afrika Magharibi, Kaskazini na Kusini.



"Ni mkutano mkubwa ambao utajadili masuala ya uongozi kwa wanawake barani Afrika wanayokutana nayo ili kupata uzoefu utakaosaidia watoto wa kike kufikia malengo yao katika kuomba nafasi mbalimbali utaona hapa Afrika kwa miaka kadhaa sasa nafasi ya Katibu Mkuu wa AU imeshikwa na wanaume pekee je hakuna Kiongozi mwanamke anayeweza kufikia huko," amesema Ndangiza.




Kwa Upande wake Kiongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya International  IDEA, Sifisisami Dube   amesema kwamba taasisi hiyo ambayo inafanyakazi chini ya mwamvuli wa ubalozi wa Sweden wakilenga kazi tatu muhimu ikiwemo kusaidia masuala ya uchaguzi, ushiriki wa kisiasa na kufanya masuala ya katiba katika nchi zinazohitaji kusaidiwa katika masuala hayo.



Amesema kuwa pia wamejikita katika kuwezesha ushiriki wa wanawake katika nyanja ya siasa pia wana kipengele cha vyombo vya habร ri vinavyojihusisha katika ajenda mbalimbali ikiwemo ushikishwaji katika siasa.

No comments:

Post a Comment