JAMII imetakiwa kushiriki katika harakati za kuwezesha wanawake kushiriki siasa kwani nafasi nyingi za uongozi kwenye siasa ndiyo zinazowezesha kuingia kwenye vikao vya maamuzi.
Hayo yamesemwa leo Juni 15, 2022 na spika wa bunge la Tanzania, Dkt, Tulia Ackson wakati akufungua mkutano wa kimataifa wa wabunge wa kikanda kutoka mabunge ya Afrika uliondaliwa na taasisi ya kimataifa ya Uongozi demokrasia usawa wa kijinsia IDEA LEAD AFRICA.
Akiongea kwa niaba ya spika Tulia, Mbunge toka bunge la Tanzania, Anastazia Wambura amesema kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana kwenye baadhi ya nchi kuweza kuwa na wabunge wengi ikiwemo Tanzania ambayo ina Rais mwanamke lakini bado kuna changamoto zinazopaswa kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Alisema changamoto zilizopo ni malezi ya watoto, wanawake ndiyo walezi na ndiyo kiungo kikubwa cha amani kwenye jamii hivyo ana majukumu mengi kifamilia na kijamii yanayomfanya anakosa muda wa kujishughulisha na maduala ya kisiasa.
"Wanawake wote ndiyo tuwe watafutaji wa hizo nafasi, jamii nzima inatakiwa ishiriki kuhakikisha kwamba wanawake wanapata nafasi katika uongozi wa kisiasa kwa sababu ndiyo sehemu maamuzi mengi yanafanyika," amesema Dkt Tulia..
Alisema changamoto zilizopo ni malezi ya watoto, wanawake ndiyo walezi na ndiyo kiungo kikubwa cha amani kwenye jamii hivyo ana majukumu mengi kifamilia na kijamii yanayomfanya anakosa muda wa kujishughulisha na maduala ya kisiasa.

Kwa upande wake, Katibu wa Umoja wa wabunge wanawake wa Bunge la Afrika mashariki, (EALA), Fatuma Ndangiza alisema kuwa mkutano huo wa siku tatu utawakutanisha kujadili changamoto za kiuongozi kwa mwanamke ili kufikia malengo ya asilimia 50/50.
Amesema pamoja na changamoto pia watapeana uzoefu utakaosaidia kuongeza wigo wa viongozi wanawake ili kufikia malengo ya azimio la Beijing la kufikia walau asilimia 30 ambapo kwa Sasa imefikiwa asilimia 25 pekee.
"Ni mkutano mkubwa ambao utajadili masuala ya uongozi kwa wanawake barani Afrika wanayokutana nayo ili kupata uzoefu utakaosaidia watoto wa kike kufikia malengo yao katika kuomba nafasi mbalimbali utaona hapa Afrika kwa miaka kadhaa Sasa nafasi ya Katibu Mkuu wa AU imeshikwa na wanaume pekee je hakuna Kiongozi mwanamke anayeweza kufikia huko," amesema Ngangiza.
Mmoja wa wadau wanaopigania haki za binadamu kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo,Agnes Sadiki alishukuru kukutana na wanawake kutoka nchi mbalimbali kwani itasaidia kuhamasisha wanawake kuwania nafasi za uongozi mbalimbali na kuweza kufanya maamuzi.
Naibu Waziri Mkuu anayeshughulika na Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda, Dk.Rebecca Kadaga alisema mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo kwa jamii ni pamoja na kuzingatia usawa katika ngazi za maamuzi hivyo ni vyema wanawake wakapewa kipaumbele.
Kwa Upande wake Kiongozi wa IDEA LEAD Afrika, Sifisisami Dube alisema kwamba Taasisi hiyo ambayo inafanyakazi chini ya mwamvuli wa ubalozi wa Sweden ambapo wanalenga kazi tatu muhimu ikiwemo kusaidia masuala ya uchaguzi ushiriki wa kisiasa na kufanya masuala ya katiba katika nchi zinazohitaji kusaidiwa katika masuala hayo.
'Lakini hii wamejikita katika kitu kimoja ambacho ushiriki wa wanawake katika nyanja ya siasa pia Wana kipengele Cha vyombo vya habà ri vinavyojihusisha katika ajenda mbalimbali ushikishwaji katika siasa," alisema Dube.
Washiriki wa Mkutano huo ni pamoja na viongozi kutoka wa mabunge ya nchi mbalimbali pamoja na kikanda ikiwemo EALA SADC ECOWAS COMESA na Afrika Magharibi Kaskazini, Kusini pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wanahabari.
0 Comments:
Post a Comment