RC AKIPONGEZA CHUO CHA IEC KWA KUSAIDIA JAMII


MKUU wa mkoa wa Arusha, John Mongela amekipongeza Chuo Cha Biblia cha kanisa la International Evangelism Center (IEC) Sakila kwa jitihada kinazofanya katika  kusaidia jamii.

Aidha amesema kuwa ataenda kukumbusha utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya ujenzi wa barabara  kwa kiwango cha lami kuelekea kijiji  ha Sakila kata ya Kikatiti wilayani Arumeru.


Mkuu wa Monduli, Fank Mwaisumbe (kushoto) akipeana mkono na Askofu  mkuu wa kanisa la IEC, Dk.  Eliud Issangya 


Hayo yamesemwa na Mongela, kwenye mahafali ya 79 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye hotuba iliyotolewa  kwa niaba yake na  Mkuu wa wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe 

Amesema kuwa anakumbuka ahadi iliyokumbushiwa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuanzia barabara kuu ya Moshi Arusha mpaka kijiji cha Sakila ambayo iliwahi kutolewa kwa nyakati tofauti Rais, Samia  na hayati Rais John Magufuli.


"Ahadi hizi hutekelezwa wakati ambapo serikali  inakuwa tayari kutekeleza nitazipeleka kwa Mkuu wa mkoa (Mongela) ili aweze kuikumbusha serikali ili iweze kutekeleza. Sina shaka kwamba serikali itafanya kama ilivyoahidi," amesema Mwaisumbe.

Amekipongeza chuo hicho kwa kuwa chachu katika kusaidia shughuli za kijamii kwa wananchi wanaoishi maeneo  kuzunguja chuo hicho huku akiwataka wahitimu kwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kujenga jamii ya watu ambao watachangia kuleta maendeleo.





Kwa upande wake, Askofu  mkuu wa kanisa la IEC, Dk.  Eliud Issangya amesema kuwa mbali ya huduma ya kiroho lakini wanatoa huduma za kijamii kupitia taasisi zao mbalimbali ikiwemo hospitali,  shule ya msingi na sekondari huku wakichimba maji kuwasaidia wananchi kupata maji safi.

 
"Tunafanya huduma za kiroho na kimwili hapa tuna mashine kubwa ya kuchimba maji tumechimbia vijiji vingi na wananchi wamepata maji safi," alisema Dk Issangya na kuongeza

...Kazi ya Mungu inaendelea na leo vijana hawa 79 wamehitimu wamekuwa wachungaji na wengine maaskofu,".

Askofu Mkuu huyo alisema kuwa Tanzania ni nchi nzuri na imebahatika kuwa viongozi wazuri walioongoza vema hivyo kuwezesha amani kudumu kwa kipindi chote  cha zaidi ya miaka 60 iliyopita baada ya uhuru.

"Mama Samia lazima tumsifu kwa uamuzi wake wa kutengeneza filamu ya The Royal Tour ili kuvutia watalii waje nchini hii ameifanya kusaidia kuinua uchumi wa Mtanzania anastahili pongezi," amesema Askofu Dk Issangya. 



Chuo hicho cha biblia kilianzishwa mwaka 1983 ambapo kimekuwa kikipokea wanachuo kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo mataifa ya Kenya, Uganda, Malawi na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.
mwishoni mwa wiki jumla ya wanachuo 79 walihitimu kwa ngazi ya Stashahada ya Uchungaji 


0 Comments:

Post a Comment