NDAKIDEMI: UJENZI HOSPITALI YA WILAYA UMEANZA

 Na Gift Mongi,Moshi



MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amesema baada ya kipindi kirefu wilaya hiyo kukosa hospitali ya wilaya sasa serikali kilio hicho kimeenda kufikia tamati baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha milioni 500 na ujenzi umeanza katika kata ya Mabogini.


Akizungumza bungeni hii leo june 23.2022 Prof Ndakidemi amesema mbali na kutolewa kwa fedha hizo tayari jitihada  za kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo umeshaanza


"Niishukuru halmashauri yangu ya Moshi imepata hati safi kwa miaka sita mfululizo niwapongeze mkurugenzi na mkuu wa wilaya pamoja na watumishi wa Halmashauri katika matumizi sahihi ya fedha za umma" Prof.  Ndakidemi 


Katika hatua nyingine mbunge huyo amesema kuwa upo uwezekano wa zao la kahawa kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa ni mkubwa japo kwa sasa limeshuka lakini bado ni zao la pili linaloingia Serikali pato la kigeni lakini Serikali ikiboresha zaidi zao hilo litaendelea kukua


" Zao la kahawa bado lina mchango mkubwa katika pato la taifa ikiwa ni pamoja na kuongeza au kuingizia taifa fedha za kigeni Sasa naona ipo haja kwa serikali kuongeza  nguvu katika uzalishaji"alisema 


Amesema pia  serikali imesikiliza kilio cha wabunge na katika bajeti ya 2022-2023 imeongeza fedha katika bajeti ya kilimo itakayosaidia kupata mbegu bora na pembejeo pamoja na kuongeza mifereji mipya na kuboresha iliyopo.



0 Comments:

Post a Comment