MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amezindua kitabu cha maisha ya Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism, Dk Elihudi Ossangya huku akimpongeza kwa ujenzi wa shule kuanzia ya awali, msingi, sekondari na chuo cha ufundi zinazotoa elimu bure.
Aidha alishukuru Askofu huyo kwa namna alivyo mstari wa mbele kuchangia jamii ambapo amechimba kisima cha maji kwenye hospitali ya wilaya ya Arumeru iliyopo Tengeru na amekuwa akikifanyia marekebisho kinapopata hitilafu.
Pia Askofu Issangya amepanga kukusanya shilingi milioni 500 kutokana na mauzo ya kitabu hicho atakazozitumia kuendelea kusaidia jamii.
Mongela ameyasema hayo Juni 22, 2022 kwenye hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi, Richard Ruyango wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika kwenye makao makuu ya kanisa hilo kijijini Sakila Kata ya Kikatiti na kuhudhuriwa na watu mashuhuri, viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Jukwaa la Maridhiano Nchini, Sheikh Musa Salum.
Amesema kuwa Dk Issangya ni mtu msikivu na mpole na amekuwa mstari wa mbele kwenye masuala ya kijamii ikiwemo kuhakikisha wanapata maji safi na salama kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan anapambana kuhakikisha wananchi wote wanayapata maji.
“Juzi nilipigiwa simu kwamba hospitali yetu ya wilaya pale Tengeru haina maji kwa sababu mota ya kupandisha maji imeungua. Kila mtu anafahamu hospitali inapokosa maji unategemea nini kuna kina mama na watoto, kuna upasuaji unafanyika nilipofika hapo nikauliza kisima hiki ni cha muda gani na ninani alikichimba nikaambiwa Dk Issagya,” alisema Mhandisi Ruyango na kuongeza.
…Sasa unajiuliza hospitali ya wilaya na huyu Dk Issangya muhubiri wa injili wapi na wapi kumbe pale tunatumia maji ,tunafulia, kazi amefanya Dk Issangya hata mafundi waliotengeneza ile mota baada ya kuungua ji wa kwake,”.
“Ni watu wachache waliofanikiwa na wakuwa na upendo kama Dk Issangya anavyofanya. Huyu ni zawadi tumepewa toka kwa Mungu na sisi tupige magoti kumshukuru Mungu tukizidi kumuombea Mungu aendekee kumlinda,”.
"Mimi binafsi Dk Issangya nilipoteuliwa alikuja ofisini naomba nimtembelee huku nilipokuja hakuwepo ila nilimuomba fedha kwa ajili ya kuwapongeza waalimu wetu. Mimi nilitazamia angechanga shilingi 20,000 lakini mchango aliotoa siwezi kusema ni mkubwa kiasi gani lakini na mimi nilipiga magoti nikasema Mungu ambariki.
Kwa upande wake, Dk Issangya amesema kitabu hicho kimeandikwa na waandishi watatu wakiongozwa na Mch Phabian Masare kwa msaada wa watu wengi wakiwemo maaskofu, wachungaji na waandishi ambao walifanya hivyo ili kuwezesha wale watakaosoma kupata maono ya utumishi wa kumtumikia Mungu.
"Tumefanya kazi tunataka Watanzania na ulimwenguni kote washuhudie jambo hilo na wajue. kazi ni moja tu ya kitabu kufungua ukurasa huo wa maandishi juu ya utumishi wetu kama watu utafikia kikomo lakini maandishi ambayo tutayaacha hayatakuwa na kikomo," alisema Dk Issangya na kuongeza.
... Yatasomwa na vizazi vijavyo hivyo kwa sababu hiyo napenda kumshukuru Mungu sana kwa kitabu hiki cha maisha yangu na huduma ya kanisa la International Avengelism Church tumetaka iwe katika maandishi,".
Askofu Issangya alirejea maandiko kwenye biblia takatifu kitabu cha Waraka wa Mtume Paulo kwa Timotheo 4:14 anayesisitiza jitihada iwekewe katika kusoma na kuandika vitabu hasa katika kufundisha.
"Ni jambo muhimu kwa kanisa na kila mmoja wetu tusome na tujifunze kupitia watu walioanza mwanzo tujue walifanyaje. Kwa mfano mimi mwenyewe katika utumishi wangu nimejifunza kuwa Yesu alikuwa wa alfajiri hakuwa analala kwa hiyo mimi kama mtumishi lazima nijifunze kuamka alfajiri na kuweka juhudi kwa kila jambo ambalo Mungu amenipangia kufanya," amesema askofu Mkuu huyo na kuongeza.
...Hivyo nilijifunza kiongozi wangu Yesu alikuwa mtu wa alfajiri na mimi nikawa mtu wa alfajiri. Hivyo na wewe unatakiwa kusoma kwa wale waliofanikiwa uweze kujifunza namna walivyofanikiwa,".
"Mtu ambaye hana mafanikio sidhani kama kuna mtu anataka kumuiga ukiwa mkulima utataka umfuatile kujifunza kwa aliyefanikiwa kwenye kilimo hata shule utajifunza kwa aliyefaulu vizuri,".
"Najua mimi ni mtu ambaye ninapenda sana kuishi kwa kuona raha duniani, sipendi mambo ya huzuni huzuni. Sipendi sana kuona marafiki au Wakristo wenzangu wanakuwa watu wa huzuni huzuni,".
Askofu Mkuu Issangya amesema kuwa wanadamu wakicheka wanapendeza sana hivyo akawasihi walioshiriki hafla hivyo kufanya mambo mema yatakayoweka kicheko kwenye nyuso zao na za wengine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa kamati ya Maridhiano, Sheikh Salum alisema kuwa kuna watu wanaishi lakini hawana jambo wanalofanya katika ulimwengu ni kama wafu.
“Lakini Askofu Dk Elihudi tunaona atakufa lakini mema yake kwa wanadamu hayatakufa kuandika ni kitu kikubwa sana hata Mwenyezi Mungu amewaweka malaika waandishi watukufu kwa ajili ya kuandika matendo yetu ili siku ya kiama uonyeshwe mambo uliyofanya ukiwa duniani,” amesema Sheikh Salum.



0 Comments:
Post a Comment