UAMUZI wa mahakama Kuu Kanda ya Arusha kubatilisha hukumu ya miaka 30 jela na kumwachia huru aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili imepokewa kwa hisia tofauti.
Wakati ndugu jamaa na marafiki wa Sabaya, Sylvester Nyegu na Daniel Bura wakifurahi, wananchi wengine wamesikitishwa na uamuzi huo wakidai kuwa Mahakama Kuu haukutenda haki kwa watu walioumizwa na tukio hilo ambao walijitokeza na kutoa ushahidi mahakamani.
Aidha, Diwani wa Sombetini, Bakari Msangi, (CCM) ambaye ni miongoni mwa walalamikaji kwenye shauri hilo amesema uamuzi huo si wa haki kwani alipigwa, kuumizwa na kuibiwa fedha zake jambo aliloeleza kusikitishwa na kuumizwa na uamuzi huo.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji, Sedekia Kisanya wa mahakama Kuu Kanda ya Musoma aliyesikiliza shauri hilo la rufaa namba 129/2021 kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha .
“Mimi nilipigwa nikanyang’anywa fedha zangu, nilifika mbele ya mahakama nikaeleza ukweli wa kile kilichotokea mahakama ikajiridhisha kuwa tukio lilikuwa ni kweli. Huu uamuzi wa kumwachia huru si wa haki ila Mungu anajua tulieleza ukweli mahakamani,” amee leza Msangi.
Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia alisema kuwa wanaenda kupitia hukumu hiyo ili wajue hatua watakazochukua.
UAMUZI
Akitoa uamuzi huo, Jaji Kisanya alisema kuwa baada ya kupitia hoja za pande mbili mahakama imejiridhisha kuna mapungufu ya kisheria kwenye mwenendo wa shauri hilo hivyo akaamuru kuachiliwa huru kwa waleta rufaa hao.
“Kwa upande wangu naona haya mapungufu ya mkanganyiko kwenye ushahidi zile ground nyingine nakubaliana na maombi ya waleta rufaa, nabatilisha mwenendo na hukumu zilizotolewa dhidi ya waleta rufaa,” alisema Jaji huyo akitoa amri na kuongeza.
“ Naamuru waleta rufani waachiliwe huru, waachiliwe huru isipokuwa kama wana mashauri mengine yasiyo na dhamana waendelee nayo,” .
Jaji Kisanya alitoa uamuzi huo kunzia majira ya saa 6 mchana ambapo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa serikali mwandamizi, Felix Kwetukia huku upande wa waleta rufaa ukiwakilishwa na mawakili Moses Mahuna, Faudhia Mustafa, Sylvester Kahunduka, Gabriel Rwahira, Edmund Ngemela na Fridolin Gwemelo.
HALI ILIVYOKUWA KABLA YA UAMUZI
Awali watu waliungia kwenye chumba cha mahakama kuanzia majira ya saa 2 asubuhi ambapo majira ya saa 4 asubuhi warufani waliingia kwenye chumba cha mahakama tayari kupoke uamuzi.
Hata hivyo majira ya saa 4:25 karani wa mahakama alitoa taarifa kuwa uamuzi huo utatolewa saa 6 mchana hivyo wanausalama waliokuwa mahakamani hapo wakawatakz watu wote kutoka nje.
Ilipofika majira ya saz 5.30 asubuhi shauri hilo liliitwa hivyo watu wakaingia kwenyE chumba cha mahakama pamoja na warufani.
SABABU ZA KUFUTA HUKUMU
Awali akichambua hoja za mawakili wa pande zote kabla ya kutoa uamuzi Jaji Kisanya alisema kuwa alipitia hoja 14 za mawakili wa waleta rufaa ambapo waleta rufaa walishitakiwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi kwa makosa matatu ya unyanganyi wa kutumia silaha.
Alieleza kuwa upande wa Jamhuri ulipeleka mashahidi 11 na vielelzo nane kuthibitisha mashitaka hayo ambapo upande wa utetezi walipeleka mashahidi sita.
“Mrufani wa kwanza (Sabaya) alieleza alienda kwenye duka la shahidi wa kwanza (Mohamed Saad) Soko kuu na alikubali kwamba kuna watu wawili aliowakamata kwenye hilo duka na kuwapeleka kituo cha polisi lakini hawakuwapiga wala kuiba kwenye hilo duka,” alieleza Jaji Kisanya akieleza mambo aliyoyasoma kwenye mwenendo wa shauri la msingi.
“Washitakiwa wawili walikana hawakuwa kwenye tukio Sylivster alisema alikuwa Bomangombe na mshitakiwa wa tatu alisema alikuwa Shamsi na akakana majina yake kuwa yeye ni Daniel Mbura na si Daniel Bura na akaleta vielelezo viwili,”.
Jaji Kisanya alisema kuwa baada ya mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mahakama iliridhika kuwa kulikuwa na kosa la kuwa unyanganyi wa kutumia silaha lakini kwa kosa la kwanza hakuona unyanganyi wa kutumia silaha lakini akaona ushahidi uliotolewa aliona ulithibitisha kosa dogo la unyanganyi wa kutumia nguvu na vile aliona likifanywa na mtu zaidi ya moja akaona walifanya unyang’anyi wa makundi (gang robbery).
Waleta rufaa wote walihukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kwanza na hayo mengine na yanaonekana yataenda kwa pamoja hivyo wakaamua kuja mahakama kuu kupinga.
Jaji Kisanya alieleza mawakili wa waleta rufaa walileta hoja 14 mahakama hapo wakipinga mahakama kuwatia hatiani wateja wao huku upande wa Jamhuri ukijibu hoja hizo.
“Hii ikiwa ni rufaa ya kwanza inakuwa katika mfumo wa kusikiliza mahakama inawajibu wa kusoma ushahidi wote na kuufanyia 'evaluation', kuanalysis kabla ya kutokea uamuzi. Masuala ya wajibu wa kuthibitisha kwenye masuala ya jinai pasipo kuacha shaka yoyote isipokuwa kama sheria imeelekeza vinginevyo huo wajibu unakuwa ni wa jamhuri na hauwezi kwenda kwa mshitakiwa,” alieleza jaji Kisanya na kuongeza.
“Katika kusikiliza rufaa hii naanza na sababu ya tatu na 11 juu ya uhalali wa mwenendo katika kusikiliza shauri hilo. Mawakili wa waleta rufaa walianisha maeneo mbalimbali ambayo wanaona mwenendo wa mahakama uliosikiliza shauri hilo haukuwa sawasawa,”.
“Kielekezo namba nne, tano na nane ilielezwa kwamba vielelezo vilipokelewa wakati kulikuwa na pingamizi mbele yake na kielelezo namba saba na nane ambavyo vilikuwa ni vya kutengeneza lakini vilipokelewa wakati vilikuwa havihusiani na shauri hilo kwa sababu vinaonyesha duka la shahidi namba moja lipo eneo tofauti na duka lilipo,”.
“Upande wa Jamhuri walisema vielelezo hivyo viko sahihi na akarejea mashauri mbalimbali yaliyowahi kufanywa na mahakama za juu.Mahakama ikisoma sheria inaona mamlaka ya kuamua upokeaji wa ushahidi iko kwenye mahakama inayosikiliza shauri hivyo mahakama ya juu haiwezi kupoke malalamiko hayo kama hayakutolewa kwenye mahakama iliyokuwa inasikiliza,”.
“Vielelezo hivyo vilipokelewa na haivikupingwa kwenye mahakama iliyosikilizwa hivyo pingamizi hilo haliwezi kuwekwa kwenye mahakama ya sasa itakuwa inakiuka taratibu kwani mahakama iliyopokea ndiyo ilikuwa ina mamlaka ya kusikiliza pingamizi hilo,”.
Jaji Kisanya aliendelea kusoma uamuzi hu kwa kusema mrufani namba tatu, (Daniel Mbura) hakuwa eneo la tukio wanadai kuwa mleta rufaa namba tatu alitoa taarifa ya kuegemea kuwa hakuwa eneo la tukio kama sheria inavyosema wanadai ilikuwa ni wajibu wa upande wa jamhuri kuonyesha kuwa mrufani wa watatu kuonyesha kuwa alikuwa.
Alisema kuwa utetezi huo ulizingatiwa na mahakama ila mshitakiwa namba tatu alishindwa kuita mashahidi aliokuwa nao siku ya tukio na huo utetezi ulipaswa kufanyiwa kwa kiwango cha mizania huku wakirejea mashauri mbalimbali ya mahakama za juu.
Jaji Kisanya alieleza kuwa upande wa Jamhuri walisema kuwa mrufani huyo wa tatu alitambuliwa kuwa alikuwa eneo la tukio hivyo mahakama ilikuwa sahihi kumtia hatiani.
“Mrufani namba tatu (Mbura) alitoa taarifa ya kutokuwa eneo la tukio na mahakama ikaangalia huo utetezi lakini haikuzingatia huo ushahidi kwa sababu mrufaa namba tatu hakuita mwanafamia au mpangaji mwenzake aweze kuthibitisha hakuwepo,” alisema Jaji Kisanya akirejea hoja za mawakili wa Jamhuri.
Alisema kuwa anakubalia na hoja za wakili wa waleta rufaa, Magafu kuwa mshitakiwa hana wajibu wa kuthibitisha hakuwa eneo la tukio ilijuwa ni wajibu wa Jamhuri kumthibitisha vinginevyo hata hivyo mahakama iliridhika kwamba huyu mrufani namba tatu alitambuliwa na shahidi namba sita (Msangi).
Kwa kuwa mahakama iliyosikiliza shauri yenyewe ilirithika kuwa mrufani wa tatu alikuwa eneo la tukio na alitambuliwa hivyo mahakama ilikuwa sahihi kumweka hatiani.
Jaji Kisanya anaeleza Mahakama ya hakimu mkazi Arusha iliyosikiliza shauri ilishindwa kuona hapakuwa na gwaride la utambulisho kwa mrufani namba moja na mbili ila upande wa jamhuri walidai kuwa mashahidi walikuwa wanawafahamu warufani namba moja na mbili hata kabla ya tukio.
Anasema dhumuni la kufanya utambuzi ni kumwezesha shahidi kumtambua mtu aliyefanyia jambo au kumvamia ambaye hakuwa anamfahamu kabla ya tukio.
"Mshitakiwa namba moja na mbili walikuwa na urafiki na shahidi namba sita, shahidi namba tano alieleza alikuwa anawafahamu mrufani namba moja kabla ya tukio hivyo hapakuwa ba sababu ya kufanya gwaride la utambulisho," anaeleza jaji Kisanya akichambua hoja za mawakili na kuongeza.
... Shahidi namba mbili na tatu , kwenye hukumu ya mahakama iliyosikiliza shauri hilo ushahidi wao haukuzingatiwa hivyo hawakuathiri kwenye uamuzi,".
"Mshitajiwa namba moja na mbili hawakukamatwa wala hawakuhojiwa kama sheria inavyotaka ila kama walifikishwa mahakama basi walikamatwa na hili la kutohojiwa la upande wa jamhuri walieleza kuwa mshitakiwa namba moja alieleza kuwa alikataa kuandika maelezo,".
"Upelelezi wa jinai unaanza baada ya kosa kuripotiwa kituo cha polisi hivyo kosa namba mbili na tatu hayakuripotiwa lakini yalipelekwa mahakamani kinyume cha sheria.
36
"Shahidi namba sita anaonekana kuwa mtu wa kwanza kuripoti tukio lililotendeka kwenye duka la shahidi namba moja na shahidi namba mbili na namba nne walikuwa wamehojiwa na shahidi namba saba ambaye alipowahoji akaona hawakuwa wamefanya uhujumu uchumi kama mrufani namba moja alivyokuwa ameripoti hivyo hoja hiyo haina msingi,".
"Mahakama ilikosea kuiruhusu jamhuri kufanya marekebisho kwenye hati ya mashitaka wakati walikuwa wameshafunga ushahidi wao. Walidai kuwa hayo mapungufu yanaenda kwenye msingi wa kesi,".
"Mrufani namba mbili Mbura na tatu, Nyegu walitaka mashahidi wa jamhuri waitwe tena jambo ambalo halikufanyika lakini jamhuri walieleza kuwa hawakuathirika kwa kuwa marekebisho yalikuwa yanahusu mabadiliko ya majina ya mrufani namba moja Sabaya na mawakili wa warufani walikuwa mahakamani na hawakuomba kuitwa kwa mashahidi hao,".
"Ni ukweli kuwa hati ya mashitaka inaweza kubadilishwa wakati wowote shauri likiendelea pale jamhuri inapoona inafaa ilimradi uamuzi haujatoka. Kwenye shauri hilo lilibadilishwa wakati shahidi wa kwanza akiwa amemaliza kutoa ushahidi wa msingi hivyo hiyo hoja haina msingi,".
Jaji Kisanya anaeleza kuwa hapakuwa na ubishi kuwa mrufani namba mbili na namba tatu waliulizwa kama watahitaji mashahidi waitwe anaweza kuwa mmoja au wote ili kutoa ushahidi upya au baadhi ya maeneo na anayepaswa kufanya hivyo ni mshitakiwa mwenyewe kwenye kumbukumbu haionyesha kama mawakili wa utetezi waliitaka mahakama iwaite mashahidi hao upya.
"Hakuna ubishi kuwa mabadiliko yaliyofanywa kwenye hati ya mashitaka kutoka Sayaba kuja Sabaya nakubaliana na wakili wa serikali kuwa mshitakiwa namba mbili na tatu hawakuathiriwa na mabadiliko hayo na waliwakilishwa na mawakili waliooaswa kuiongoza mahakama kufanya hayo.

No comments:
Post a Comment