ONGEZEKO BEI YA MAFUTA, WAFANYABIASHARA WATAKA WATAKA TOZO ZIONDOLEWE

WADAU sekta za Utalii, Usafirishaji, viwanda na kilimo wameishauriwa serikali kupunguza kodi, tozo na ushuru ilizoweka kwenye mafuta ili bei ya mafuta iliyopanda kuanzia Mei 4, mwaka huu ipungue.


Aidha wamedai  ongezeko hilo la bei ya mafuta mbali ya kuwa na athari ya moja kwa moja kwenye biashara zao lakini serikali nayo itaathirika kwani itakusanya mapato kidogo ya kodi kutokana na kudorora kwa biashara.


Wadau hao waliayasema hayo jana kwa nyakati tofauti wakati wakiongea na Tanzania Daima juu ya ongezeko hilo la mafuta lilitangazwa Mei 3, mwaka huu na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, (UWURA).


Walisema kuwa ongezeko hilo  lina athari kubwa kwenye biashara zao kwani inafanya gharama za uendeshaji kuwa juu jambo litakalowalazimu na wao kuwatoza kiasi kikubwa wateja wao jambo litakalofanya kasi ya biashara kushuka hivyo kuathiri hata makusanyo ya kodi ya serikali.



Mwenyekiti wa Chama Cha wasafirikisha mikoa ya Kilimanjaro na Arusha,(AKIBOA), Locken Adolf Massawe alisema kuwa kiwango kilichotangazwa kupandishwa ni kikubwa ambapo alishauri serikali kupunguza tozo na kodi walizoweka kwenye bidhaa hiyo ili kuwapa unafuu wananchi. ambali ya


 


“Inashangaza kuona EWURA wanatangaza kupandisha bei leo na siku inayofuata utekelezaji unaanza bila kukusanya maoni. Sisi LATRA (Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini)  wametafuta ushauri na maoni ya wadau wametuongezea nauli ya shilingi 100 wametuambia tusubiri mpaka tarehe 15 ndiyo nauli mpya zitaanza kutumika,” alisema Massawe na kuongeza.


 


.. Ukipakia abiria 30 kwenda Moshi kutoka Arusha nauli yao utakusanya  shilingi 90,000 na ukiweka mafuta lita 30 tu ni shilingi 94,000 ukiangalia gharama nyingine utaona namna biashara inavyokuwa ngumu,” .


“Sisi (wasafirishaji) hatuwezi kuongeza bei, bei wanatuongezea LATRA yaani sisi tumebanwa kila upande mafuta hayajapanda kwa kiwango hicho kwenye soko la dunia wao wanapandisha kwa jinsi wanavyotaka bila maoni bila ushauri wa sisi wadau,”



Serikali inatakiwa kuelewa kupanda kwa bei ya mafuta hata uchumi utayumba kwani mzunguko wa biashara utakuwa mdogo kwani mtu ataona kuliko atumie ghari binafsi aweke mafuta lita tatu kwa shilingi 10,000 ni bora apande usafiri wa umma kwa shilingi 500,” alisema Mfanyabishara mwingine ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.




Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo, (TCCIA), mkoani Arusha  Walter Maeda alisema kuwa huenda  wafanyabiashara wakashindwa kuendesha kazi kwa ufanisi  sababu kila kitu kitapanda bei ikiwemo bei za bidhaa na huduma kwani vyote vinategemea mafuta ya usafirishaji.


 


“Ongezeko la shilingi 485 kwenye mafuta ni kubwa sana wanasema ni kwa sababu bei imepanda kwenye soko la dunia,  sisi tunaiomba serikali itufikirie kwa kupunguza kodi na tozo,” alisema Maeda na kuongeza


…Kuna tozo nyingi sana kwenye mafuta tozo za serikali zipo karibu 15, tunaomba zipunguzwe ili na sisi tupate unafuu hili ongezeko la karibu shilingi 500 ni kubwa sana,”.


 


Kwa upande wa sekta ya Utalii, inadaiwa kuwa ongezeko hilo litakuwa na madhara ya moja kwa moja kwa makampuni ya uwakala wa utalii kwani wao huchukua fedha za wageni mapema hata mwaka mmoja kabla wageni hawajafika.


“Wageni watapungua sana,  ukiwaambia wageni bei imeongezeka kwa sababu bei ya mafuta imepanda kuna watakaoelewa na wengine hawataelewa wanaweza kuamua kufuta safari,” alisema mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya uwakala wa utalii ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.


…Unajua wangekuwa wameongeza bei kidogo walau unaweza kumuongezea mgeni ukimuelewesha inakuwa rahisi kuelewa ila kiwango cha zaidi hya shilingi 400 ni kikubwa sana,”.


“Mgeni anayekuja Julai mwaka huu alishafanya maandalizi ya safari tokea mwezi Aprili mwaka jana. Unakuta tumeshamuandalia safari yake ikiwemo hoteli na kulipia kuingia hifadhini hata tiketi ya ndege wameshalipia sasa kuanza kumweleza bei itaongezeka ni changamoto,” .


“Tuishauri serikali iondoe tozo lukuki kwenye  mafuta hizi ndiyo zinafanya bei inakuwa juu,  ipunguze hivi vyombo vinavyosimamia mafuta ambavyo inabidi waweke tozo kwenye mafuta ili viweze kujiendesha,” .



 

0 Comments:

Post a Comment