Thursday, May 26, 2022

NMB WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI, BARABARA ZAFUNGWA


BENKI ya NMB tawi la Clock Tower wamefanya zoezi la utayari ambapo vikosi vya polisi vilitanda huku barabara zote zinazelekea ilipo benki hiyo karibu na mzunguko wa mnara wa saa zikifungwa kwa muda.



Tukio hilo lilitokea leo Mei 26, 2022 majira ya ambapo  meneja wa NMB wa tawi hilo, Emmanuel Kishosha alisema kuwa  lilikuwa ni zoezi la utayari ambalo hufanyika kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya kupima utayari wa wafanyakazi, wateja na vyombo vya uokoaji katika kujiokoa na kuokoa watu na mali zao.


Meneja huyo amevishukuru vyombo vyote vya uokoaji vilivyofika na kusaidia kuokoa na kuzima moto huo kwa wakati wakiwemo jeshi la polisi, zima moto, TanESCO, hospitali ya mkoa ya Mount Meru na wadau wengine walioshiriki zoezi hilo.


"Ni vizuri watu kukata bima ya moto kwani kama benki ya NMB mali zote ziko salama na fedha za wateja wetu zote ziko salama unaweza ukapata janga la moto ukajilinda lakini bima ikakufidia madhara yaliyotokana na moto huo, amesema Kishosha na kuongeza.

"Naomba nitoe taarifa hii, tukio la leo tumefanya ni tukio la utayari wa kuzima moto unaweza kutokea muda wowote lakini ni vizuri kama wateja au wafanyakazi  kuhakikisha tunakuwa tayari muda wote.,". 

"Tunafanya mazoezi haya kwa mujibu wa sheria kuhakikisha tunakuwa salama muda wote naomba niwahakikishie tena hili zoezi la leo likikuwa ni kwa ajili ya utayari endapo tukio la moto lingetokea kwenye eneo letu,".

Kwenye tukio hilo majeshi ya polisi na uokoaji na zima moto walikuwa wa mwanzo kufika kwenye benki hiyo na kuweka utepe kuzuia watu wasisogelee huku juhudi za kuzima moto huo kwa poda maalum uliendelea.

Hata hivyo shirika la umeme nchini, (TANESCO) ambao ofisi zao za mkoa ziko mita chache kutoka ilipo benki hiyo walifika kwa uchelewa .

Wakiongelea sababu za kuchelewa huko, kaimu meneja wa mkoa na mkuu wa kitengo cha dharura ambao hawakuwa tayari majina yao yanukuliwe walidai kuwa mwenye mamlaka hayo ni meneja wa mkoa, Mhandisi Herini Mhina ambaye hakuwa ofisini.



"Sisi hatukupewa taarifa yoyote hata ukiangalia kitabu chetu cha taarifa za  dharura hautaona hiyo taarifa. NMB hawakutupigia simu hivyo sisi tulijiongeza tu tukaamua kwenda na mnaposema kuchelewa mnazingatia nini," amesema kaimu meneja huyo.

Hata hivyo aliwaelekeza waandishi wa habari kwenda kwa mkuu wa kitengo cha dharura ambaye naye alidai kuwa yeye aliposikia king'ora cha zimamoto aliamua kumpigia kamanda wa kikosi hicho lakini hakupokea hivyo hakujua mara moja moto huo uko eneo gani.

 
Shuhuda wa tukio hilo, Rose Mbise amesema kuwa wao walikuwa ndani kwenye foleni ndani ya benki kukawa na mlio wakawa hawajui nini kimetokea kisha wakaona askari wanazunguka wanapanda juu na kushuka.

"Askari akasema kuna moto watu wote tokeni nje ndiyo tukaona watu wengine wanaanguka wengine wanazimia kulikuwa na moshi uliokuwa unatokea kwa kule juu," alisema Mbise huku akiwa na hofu..

Kwa upande wake, Mkuu wa kikosi cha uokoaji na zima moto mkoa wa Arusha, Oswald Mwanjenjele amesema kuwa moto huo ulianzia kwenye eneo la juu kunakotunziwa fedha ambapo walipigiwa simu majira ya saa 6:37 mchana wakiambiwa moto umeanza na walifika saa 6:48 wakaanza kuuzima.

"Tumeokoa watu watano walioonekana wamejeruhiwa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wanapatiwa huduma... tumefanya kazi yetu vizuri tumeokoa watu na tumezima moto na eneo liko salama," amesema 

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Mary Kipesha, amesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme ambapo wao kama polisi walifika eneo hilo dakika tano baada ya kupata taarifa kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao.


"Tuliwatahadharisha wananchi waliokuwa wanakimbilia eneo la tukio wakato sisi tunajua ni eneo hatarishi hivyo tuliweka alama ili kuhakikisha watu waliokuwa ndani wanatoka wakiwa salama na walio nje wanakuwa salama,".




No comments:

Post a Comment