Amesema kuwa ili kusudi hilo litimie lazima wahubiri Injili kupitia utumishi waliopewa hivyo wakafanye kazi hiyo kwa ukamilifu ili waongeze waumini na wahakikishe injili hiyo inafika vijijini.
Akizungumza mara baada ya kuingizwa rasmi kazini Askofu Dr Philemon Langas Molel amesema kuwa kanisa hilo linamhubiri Yesu Kristo kama ilivyo kwa makanisa mengine isipokuwa kanida hilo halibariki wanawake kuwa wachungaji.
Kwa upande wake msaidizi wa Askofu mchungaji Dr Philemon Olaisi Molel (MONABAN) amesema kuwa Mungu amempa vipawa viwili ikiwemo Cha Siasa pamoja na utumishi wa madhabauni hivyo atavitumia vyote kwa pamoja.
Amesema kwa kuwa atawahidumia watu wake kiroho na kimwili na atahakikisha anavitumia vizuri Kama Mungu alivyokusudia.
‘Kanisa letu tutakuwa tunahubiri upendo amani, ushirikiano na umoja katika maeneo yote nchini na hata kwenye nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki,”amesema Dk Monaban
Naye , Katibu wa KKAM, Heroki Mkwizu amesema kuwa parokia nyingi kwa Sasa zitafunguliwa Arusha pamoja na maeneo mengine Mara baada ya kuongezeka kwa watumishi hao.




No comments:
Post a Comment