Mawakili wa Chadema katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Mawakili hawa waliosimama mahakamani kuwatetea wanachama wa Chadema katika kesi mbalimbali wamepewa medali maalum na kuvalishwa na mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe katika kikao cha Baraza Kuu leo Mei 11, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City.
Wakili Peter Kibatala apewa tuzo maalum iitwayo Justice and Freedom. Imepokelewa kwa niaba yake na wakili John Mallya.
![]() |
Msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini, Sisty Nyahoza akiongea katika Baraza Kuu la Chadema amesema, uwepo wa vyama vingi kushiriki katika baraza hilo ni ishara tosha ya ushirikiano wa chama hicho na vyama vya siasa huku akiwataka kuzingatia katiba ya nchi na ya chama chao.


No comments:
Post a Comment