GCLA YAUZA KEMIKALI ILIYOTAIFISHWA




MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Kanda ya Kaskazini imeuza kwa mnada wa wazi wa madumu 170 yenye lita 250 kila moja za kemilika aina ya Ethly kwa Kampuni ya Rastonty Enterprises Ltd ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mnada huo umefanyika leo Mei 9, 2022  kwenye ofisi za kanda za GCLA zilizopo jijini Arusha aambapo kemikali yote italipiwa jumla ya shilingi milioni 68 kulingana na bei iliyouzwa kwenye mnada huo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Rastonty Enterprises LTD, Joyce Mugendi ameishukuru serikali kwa kutangaza mnada huo na kufanya kwa haki na uwazi huku akiahidi kuwa wataiuza kwa watu na taasisi zilizosajiliwa kutumia kemikali hiyo.


"Sisi Leo tumeshinda kwa kununua dumu moja kwa  Sh.400,000 ambapo leo tumelipa asilimia 25 ya fedha zote kama sheria inavyotaka na ndani ya siku 14 tutamaliza fedha zote tunazotakiwa kulipa," amesema Mugendi na kuongeza.

"Sisi kwa kemilikali  hii tunaenda kuuzia wanatengeneza pombe kali za aina mbalimbali wanaotambulika na serikali na siyo vinginevyo,".

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za sheria GCLA, Gilbert Ndeoruo amesema, mshindi wa mnada huo ameshinda kwa kukubali kununua kila dumu moja kwa Sh.400,000 ambazo anatakiwa kulipa asilimia 25 ya fedha zote na inayobaki atamalizia ndani ya siku 14.


Amesema magumu hayo yalipatikana mwaka jana baada mfanyabiashara mmoja ambaye hakumtaja jina kukamatwa akiingiza kemikali hiyo bioa kuwa na vibali vya GCLA hivyo akashitakiwa na mahakama ikaamuru yataifishwe na serikali.



"Sisi tulimkamata na kumfikisha mahakamani na tulishinda kesi kwa mahakama kuamuru madumu haya kutaifishwa na serikali baada ya kubaini muhusika aliingiza nchini kinyume na sheria na leo tumepiga mnada na kupata fedha hizi," amesema Gilbert



Alitoa wito kwa watu wote wanataka kufanya biashara hiyo,wahakikishe wanafika kwenye ofisi GCLA  ili wapewe utaratibu na elimu juu ya uagizaji, uingizaji na utumiaji,kwa ajili ya kuwasaidia kuepuka hasara wanayowezs kuosta endapo wataenda kinyume na sheria hivyo kujikuta wanaingia kwenye mikono ya serikali.



Kwa upande wake Meneja wa GCLA  Kanda ya Kaskazini, Christopher Anyango,amesema kazi yao kulinda kemilikali zote zinazoingia nchini,sababu zisipotumika vyema zinaweza kuleta athari kwenye afya za watu na mazingira.


"Hivyo lazima sisi tuwasajili na kukagua pamoja na kutoa vibali na elimu, tunaamini anayesajili atakuwa amelazwa namna salama ya kutumia kemikali hii,ili kutoleta athari za afya na mazingira na hii ni mojawapo ya matumizi ya viwandani,tusipodhibiti inaweza leta athari kubwa katika maeneo hayo," amesema Anyango.


Amesema kemikali hiyo inaweza  kutumika kutengeneza  vinywaji vya pombe kali (spirit) isipotumika Kwenye hiyo kazi ilivyokusudiwa ikatumika maeneo mengine inaweza kusababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo kuleta upofu na kuharibu mapafu.




0 Comments:

Post a Comment