Thursday, May 12, 2022

BARAZA KUU CHADEMA LILIVYORIDHIA WABUNGE 19 KUTIMULIWA


BARAZA kuu la Chadema limeridhia maamuzi ya Kamati kuu ya chama hicho ya kuwafutia uanachama waliokuwa wabunge 19 wa chama hicho kwa kura 413 kati ya 423 
zilizopigwa .


Aidha kati ya kura hizo 5 zilikuwa za hapana na 5 zisizofungamana na upande wowowte huku kukiwa hakuna hata moja iliyoharibika.

Mkurugenzi wa itifaki na mawasiliano wa chama hicho, John Mrema amesema kuwa baada ya uamuzi huo Katibu Mkuu wa CHADEMA, ataandika barua kwenda ofisi ya spika kumtaarifu uamuzi huo.

"Suala hili limegitimidhwa na hili litafanyika haraka na tutamwachia sasa spika afanye uamuzi kama alivyosema anasubiri rufaa," amesema Mrema.


Kura za Ndiyo 413 sawa na asilimia 97.6, kura za hapana , 5 sawa na asilimia 1.2  na kura za wasiokuwa na upande 5 sawa na asilimia 1.2 huku kukiwa hakuna zilizoharibika.





MATOKEO KWA KILA KANDA

Kanda ya Victoria wajumbe 44, Wanaokubalia wavuliwe uwanachama 42,Wasiokubali 1,-Wasiofungamana na Upande  wowote 1


Kanda ya Nyasa Wajumbe 57, wanaokubali wavuliwe uanachama 57, wasiokubalina 0, wasifungamana na Upande wowote 0. 

Kanda ya Unguja Wajumbe 22, wanaokubali wavuliwe uanachama 19, wasiokubali 1, wasifungamana na Upande wowote 1.

_

*Kanda ya Pemba 15*
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 12
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 2
_*Jumla ya Kura 15*_

*Kanda ya Kusini 32*
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 32
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
_*Jumla ya Kura 32*_

*Kanda ya Pwani 47*
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 45
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 2
_*Jumla ya Kura 47*_

*Kanda ya Kati 44*
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 44
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
_*Jumla ya Kura 44*_

*Kanda ya Serengeti Wajumbe 41*
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 41
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
_*Jumla ya Kura 41*_

*Kanda ya Magharib Wajumbe 37*
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 37
Wasiokubali 0
Wasifungamana na Upande wowote 0
_*Jumla ya Kura 37*_

*Kanda ya Kaskazini Wajumbe 61*
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 61
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
_*Jumla ya Kura 61*_

Kura za Kamati Kuu 23
Wanaosema wavuliwe 23
Wasio kubali 0

Matokeo  kura zilizopigwa   423:
Ndio 413
 Hapana 5
Wasio kuwa na upande 5
Jumla 423

No comments:

Post a Comment