RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua filamu ya kuhamasisha na kutangaza vivutio vya utalii nchini, maarufu The Royal Tour, jijini Arusha Aprili,28 mwaka huu
Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela, ameyasema hayo leo April 23, 2022 kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa,AICC,alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuelezea hatua ya maandalizi ya uzinduzi wa filamu hiyo.
Amesema kuwa Rais, Samia ambae kwa sasa yupo nchini Marekani,atawasili Arusha April 28 asubuhi na mchana atafanya uzinduzi wa filimu hiyo kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC.
"Mkoa wa Arusha, umepewa heshima kubwa ya kuwa mwenyeji wa shughuli hiyo ya kuzindua filamu hiyo na hilo ni jambo la kitaifa na kihistoria baada ya filamu hiyo kuzinduliwa April 18 Jijini Newyork na baadae April 21 Jijini Los Angeles nchini Marekani na April 28 uzinduzi unafanyika Jijiji Arusha," amewsema Mongela.
Amesema kuwa katika uzinduzi huo kutakuwepo wageni na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini, wawekezaji, wadau wa utalii na uhifadhi, wafanyabiashara pamoja na wananchi.
Mongela amesema Idadi ya watalii wa ndani anaotembelea hifadhi mbalimbali nchini imeongezeka kutoka 562, 549 mwaka 2020 hadi kufikia watalii 788,933 mwaka 2021
Aidha baada ya UVIKO 19 idadi ya watalii kutoka nje ya nchi imeongezeka kutoka 620, 867 mwaka 2020 hadi kufikia watalii 922,692, mwaka 2021.
Mongela amesema filamu hiyo inatarajiwa kuongeza chachu na mwitikio mkubwa zaidi kwa wageni watakaotembelea nchi yetu kwani mara baada ya kurekodiwa na kuanza kurushwa kuna dalili za kuwepo ongezeko la watalii ambapo wiki iliyopita kundi la watalii kutoka nchini Israel wamekuja nchini.
Filamu hiyo imerekodiwa katika hifadhi za Taifa za Mlima Kilimanjaro(KINAPA) na Serengeti, (SENAPA), Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro , (NCAA) na eneo la uchimbaji wa madini ya Tanzanite la Mirerani lililopo mkoani Manyara.
Uzinduzi rasmi wa kwanza wa Royal Tour ulifanyika nchini Marekani kwenye jijini New York April 18, mwaka huu kisha kufuatiwa na Los Angeles April 21, mwaka huu

No comments:
Post a Comment