Wednesday, March 16, 2022

TAREHE HUKUMU KESI YA SABAYA KUJULIKANA MACHI 31

  


MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga kukutana Machi 31, 2022 wa ajili ya kutangaza tarehe ya kutoa ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.




Aidha imetoa siku 14 kwa mawakili wa pande zote na mshitakiwa wa tatu anayejitetea mwenyewe, Watson Mwahomange wawe wamewasilisha hoja zao za majumuisho.


Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27/2021 ameyasema hayo leo Machi 16, 2022 mara baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wao.


"Mahakama imekubali ombi la kuwasilisha hoja za majumuisho ya mwisho kwa siku 14. Machi 31, hoja hizo ziwe zimeshawasilishwa. Siku hiyo kesi itatajwa kwa ajili ya kutangaza tarehe ya hukumu,” amesema hakimu Kisinda.


Awali, mara baada ya  ya shahidi wa nane, Nathan Msuya kumaliza kutoa ushahidi wake mahakamani hapo, wakili wa utetezi, Mosses Mahuna aliomba mahakama iwapatie fursa ya kuwasilisha hoja za majumuisho kwa maandishi.



"Kwa kawaida ni kuiachia mahakama kwa ajili ya kutupatia tarehe ya hukumu lakni kabla mahakama haijatamka tarehe tulikuwa na ombi upande wa utetezi ambalo kama litaridhiwa na Jamhuri tufanye majumuisho ya mwisho ambayo yataisaidia mahakama kufanya uamuzi wake," ameomba Mahuna na kuongeza.



....Mheshimiwa kama aombi litaridhiwa na mahakama yako tulikuwa na ombi mawasilisho ya mwisho kwa pamoja ndani ya kipindi kisichozidi siku 14, na nimezungumza kwa niaba ya washitakiwa wote isipokuwa mshitakiwa wa tatu,".


Kwa upande wa Jamhuri, wakili wa serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga alisema kuwa hawana pingamizi na wako tayari kuwasilisha hoja hizo kwa njia ya maandishi.


Kwa upande wake mshitakiwa wa tatu, Mwahomange naye alisema kuwa atawasilisha hoja hizo kwa maandishi.


Shauri hilo linalofuatiliwa na wengi lilifika mahakamani Juni, 2021 ambapo upande wa jamhuri walileta mashahidi 13 na vielelezo huku upande wa utetezi ukiketa mashahidi saba.



Mashahidi wa utetezi walikuwa ni washitakiwa wenyewe pamoja na mke wa Sabaya, Jesca Nassari

No comments:

Post a Comment