Daraja jipya la kisasa linalokatiza kandokando ya bahari ya hindi katika jiji la Dar e salaam nchini Tanzania limezinduliwa huku kukiwa na matumaini ya kupungua foleni katika jiji hilo la kibiashara.
Akizundua daraja hilo leo Machi 24, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kusisitiza kwamba serikali anayoiongoza atahakikisha inakamilisha miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake Hayati Rais Magufuli.
Daraja hilo la Tanzanite lililopo Jijini Dar es Salaam lenye urefu wa kilomita 1 na mita 30 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 5.2.
Mradi huu pia ulianzishwa wakati wa utawala wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Rais John Pombe Magufuli mwaka 2018.
Samia amesema miradi ya barabara katika Majiji na Miji mbalimbali nchini ikiwemo Jiji la Dodoma na Dar es Salaam itakamilika ili kurahisisha usafiri nchini, amewataka Watanzania wote kuhakikisha wanayatunza madaraja na barabara zinazojengwa nchini kwani serikali inatumia pesa nyingi kuijenga miundombinu hiyo.
Amesema daraja hilo lililojengwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limebadirisha mandhali ya Jiji la Dar es Salaam lakini pia limesaidia kutatua changamoto ya msongamano wa Magari katika eneo hilo ambalo awali lilikuwa na msongamano wa Magari katika daraja la Salenda.
Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema daraja hilo ambalo limepewa jina la Tanzanite ni vema likawekewa alama ya Tanzanite ili kufasiri jina la daraja hilo.
Ameishukuru serikali ya watu wa Korea kwa kuishika mkono serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini ukiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la Tanzanite.



No comments:
Post a Comment