SAMIA ARIDHIA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA KUUZIWA WAPANGAJI


RAIS, Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wakazi wa Magomeni Kota kuuziwa nyumba kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi huku akiwataka waliokuwa tayari kuanza kulipia mara moja.



Ameridhia hayo leo Jumatano Machi 23, 2022 wakati akizindua nyumba hizo nyumba 644 za waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota Kinondoni.

Katika uzinduzi huo, Rais Samia amefafanua kuwa wakazi hao watatakiwa kurejesha gharama za ujenzi pekee na hawatozwa gharama ya ardhi ili wapate nafuu za kuzinunua.

“Nimeridhia wananchi hawa kuuziwa nyumba kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi na kurejesha gharama za ujenzi pekee, hatutawatoza gharama za ardhi kwasababu tukifanya hivyo mtashindwa,” Amesema Rais Samia na kuongeza.


...Kwa wale wanaotaka kulipa polepole, wanaweza wakaanza sasa mchakato huo ili ikifika miaka mitano, kama umemaliza au unaendelea kulipa na kubaki katika nyumba. Mnaweza kuanza kulipa sasa na mkianza wote kwa pamoja itakuwa vizuri zaidi, niwaombe muanze kulipa sasa,”amesema Rais Samia.


Amewaasa wananchi hao kuanza kulipa fedha polepole ili Wakala wa Majengo Tanzania,(TBA) wapate fedha za kumalizia palipo bakia.


“Mnaweza kuanza kulipa sasa na mkianza wote kulipa sasa itakuwa vizuri zaidi kwasababu mtawasaidia TBA wakusanye fedha ya kumalizia eneo lililobakia kwaiyo niwaombe sana muanze kulipa sasa,” amesisitiza  Rais Samia.


Awali mwakilishi wa wakazi 644 wa Magomeni Kota, George Abel amedai kuwa asilimia 80 ya wakazi wa nyumba hizo ni wazee, wajane na kipato chao cha chini.


 “Mama ameagiza katika zile huduma muhimu hatutalipia ndani ya miezi mitatu. Pia tutakaa miaka mitano bure. Leo umetufuta machozi, hayawi hayawi sasa yamekuwa,”amesema Abel.


Mradi wa magomeni kota ulianza mwaka 2016 katika awamu ya tano chini ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 52 ambapo kila jengo linabeba kaya 128.

zilizojengwa kwa Sh51 bilioni na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mchakato wa ujenzi huo ulianza 2016 na kukamilika mwaka huu.

0 Comments:

Post a Comment