WATU saba wamefariki na wengine nane kujeruhiwa baada ya lori kugongana uso kwa uso na bajaji hivyo kusababisha bajaji hiyo kuungua moto huku watu waliokuwa juu ya lori hilo kufunikwa na matofali.
Ajali hiyo imetokea Machi 27, 2022 eneo la Kidulya nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, ikihusisha lori lenye namba za usajili T 172 AUP lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 471 ABT lilikuwa limepakiwa matofali likitokea barabara ya Luguru kwenda mjini Bariadi.
Inadaiwa lori hilo lililogongana uso kwa uso na bajaji wakati likijaribu kuipita trekta hivyo kukutana uso kwa uso na bajaji.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Simiyu, Faustine Mtitu amenukuliwa na vyombo vya habari akisema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa lori uliosababisha kugonga bajaji.
"Baada ya lori hilo kuigonga bajaji inayokisiwa kuwa ilikuwa imebeba abiria sita na lori likiwa na watu takribani 12, bajaji iliwaka moto na lori kupinduka," amesema Mtitu.
Kaimu Mganga Mkuu halmashauri ya mji wa Bariadi Marco Igenge amesema ajali hiyo imetokea marchi 27 (saa 1:00 jioni) ambapo walipokea majeruhi na miili marehemu majira ya saa mbili kasoro usiku na kwamba hali za majeruhi zinaendelea vizuri.
Wakielezea tukio hilo, baadhi ya majeruhi Manjale Kasule wamesema walikuwa nyuma ya tela lililokuwa likikokotwa na Lori na ndani lilikuwa na matofali na baada ya Lori kukwepa trekta na kuigonga bajaji trekta lilianguka na matofali yakawafunika.
Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wanadai chanzo kikubwa cha ajali ni trekta.

0 Comments:
Post a Comment