JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wanawashikilia mwandishi wa mkurugenzi wa Mtandao wa Kijamii wa U-turn Connection, Samuel Mhina,
mkazi wa Temeke na wenzake 13 kwa tuhuma za kusambaza video za aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na mwanamuziki maarufu, Joseph Haule ‘Prof Jay’ akiwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kibali cha hospitali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Machi 17, 2022 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema
watuhumiwa hao walikutwa na vifaa mbalimbali vya kielektroniki, ikiwemo kamera, kalamu za kiuchunguzi, miwani na kofia zenye camera, laptop na memory card ambavyo vyote vinachunguzwa na mamlaka husika ili kubaini uhusika wake na tukio la kusambazwa kwa video hiyo ambapo uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.
0 Comments:
Post a Comment