Wednesday, March 23, 2022

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI HATARINI KUKUMBWA NA NJAA KUTOKANA NA VITA UKRAINE


Watu karibu milioni 28 Afrika Mashariki wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa kulikosababishwa na vita vya Ukraine na ukosefu wa mvua mwezi huu wa Machi, shirika la Oxfam limeonya.

Kenya, Somalia na Ethiopia zinakabiliwa na hali mbaya ya hewa katika kipindi cha miaka 40, wakati huo huo Sudan Kusini inakabiliwa na mafuriko yanayoendelea, Shirikia hilo limesema.

Pia Shirikia hilo iliangazia kile inachokiona kama kuisumbua Jumuiya ya kimataifa kwa sababu ya mgogoro wa Ukraine, na kusababisha kupuuzwa kwa matatizo ya chakula katika kanda ya Afrika Mashariki.

Kuhusu hatua za kimataifa zilizochukuliwa mpaka sasa , taarifa kwa vyombo vya habari ya shirika hilo ilisema kuwa ni asilimia 3 tu pekee ya dola bilioni 6 (£4.5bn) kutoka mpango wa Umoja wa Mataifa (UN) wa 2022 ndizo zilizotoka kusaidia Ethiopia, Somalia na Sudan Kusini.

"Maeneo ya Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini na kwingineko yanakabiliwa na janga kubwa zaidi linalojitokeza sasa. Hata kama mvua zitanyesha mwezi huu, ahueni haitaonekana isipokuwa kama hatua za haraka zitachukuliwa leo, "Mkurugenzi Mtendaji wa Kimataifa wa Oxfam, Gabriela Bucher, alionya.

Athari za mgogoro wa Ukraine kwenye mfumo wa chakula duniani zitabadilika duniani kote, lakini ni watu maskini zaidi na walio katika mazingira magumu zaidi ambao watakuwa miongoni mwa wale waakaoathirika zaidi na kwa kasi zaidi, "aliendelea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nchi za Afrika Mashariki zinapata hadi asilimia 90 ya ngano yao kutoka Ukraine na Urusi.

Mkulima mmoja alisema ukosefu wa chakula na maji unaathiri mifugo yake: "Kutokana na ukame ambao punda wetu wameangamia na wale waliobaki ni dhaifu sana kuweza kuvuta mikokoteni," Ahmed Mohamud Omar kutoka Kaunti ya Wajir, Kenya, alisema.

"Nafikiria kuhusu nini familia yangu itakula, chakula chao kijacho kitatoka wapi, je nitapata maji ya kila siku," aliendelea.

Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment